WAISLAMU KATAVI WATAKIWA KUWA WAMOJA NA WENYE MOYO WA HURUMA-Septemba 1,2017
WAISLAMU mkoani Katavi wametakiwa kuwa
wamoja na wenye mshikamano katika hali mbalimbali ya maisha ya kila siku
wanayopitia bila kujali itikadi ya chama,rangi,dini,kabila wala taifa analotoka
kwa kuwa wote ni binadamu ambao wameumba na mwenyezi mungu.
Wito huo umetolewa na Kaimu shehe
mkuu wa Mkoa wa Katavi Shehe Nassoro Kakulukulu,katika swala ya baraza la Eid ambayo
imeswaliwa katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili.
Aidha Shehe Kakulukulu ambaye pia ni Mjumbe
wa baraza la mashehe Mkoa na mjumbe wa Halmashauri kuu taifa amesema,waislamu
wanatakiwa kuvumiliana kwa sababu mungu ameumba watu mbalimbali wenye fikra na
akili tofauti.
Kwa upande wake Khershah Fazal ambaye
ni Mwenyekiti wa mkoa wa Katavi wa taasisi ya Markaz Tabligh yenye makao makuu Kiwalani
Jijini Dar es salaam amesema,waislamu wanatakiwa kupendana,kusaidiana na
kuoneana huruma wao wenyewe wakati wa shida pamoja na kuzingatia amri za
mwenyezi mungu kwa vitendo.
Sala ya baraza la Eid ya mwaka 1438
wa kiislamu ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wakiwemo katibu wa bakwata
Wilaya ya Mpanda Shehe Omary Muna,wajumbe wa baraza kuu ngazi ya taifa,mashehe
wa misikiti ngazi ya mitaa,wilaya na mkoa.
Comments