SITA WAHUKUMIWA MIAKA 20 JERA KWA JARIBIO LA KUUA,YUMO MWENYE UALBINO ALIYEKATWA MKONO-Septemba 1,2017
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya
Sumbawanga imewahukumu washtakiwa sita kati ya
kumi kifungo cha miaka 20 jela baada ya kuwatia hatiani kwa makosa
mawili ya kula njama ya kuua na jaribio la kumuua mtoto mwenye ulemavu
wa ngozi ‘albino” Mwigulu Matonange (13) kwa kumkata mkono wake wa
kushoto .
Hukumu hiyo ambayo imesomwa leo
mahakamanki hapo imevuta hisia ya wakazi wa Mji wa Sumbawanga akiwemo
Mkuu wa mkoa wa Rukwa,Zelothe Steven aliyehudhuria na kusikiliza hukumu
hiyo hadi mwisho.
Akisoma hukumu hiyo Jaji wa mahakama
Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga Dk Adam Mambi pia aliwaachia
huru washtakiwa wanne baada ya upande wa mashtaka
kushindwa kuthibitisha bila kutia shaka yoyote makosa yao .
Waliohukumiwa kutumikia kifungo
cha miaka 20 jela kila mmoja ni pamoja na Weda Mashilimu
“Baba Siha ,Ignas Sungura , James Paschal , Nickson Ngalimia Ibrahim Tela na
Faraja Jailos “Mwezi mpya “.
Walioachiwa huru ni pamoja na Kulwa
Mashilimu,Peter Said“Simon Msalaba”,Hamis Rashid na James Ngalamio.
Jaji Dk.Mambi alisema washtakiwa
sita walitenda makosa hayo kinyume na kifungu cha
215 cha kanuni ya sheria ya adhabu Sura namba 16
iliyofanyiwa marekebisho 2002 na Kifungu 211 cha kanuni ya sheria ya
adhabu .
“Katika
kosa la kwanza la kula njama ya kuua adhabu yake
ni kifun go cha miaka 14 jela na kosa la pili la
jaribio la kuua adhabu yake ni kifungo cha maisha
lakini mahakama kwa kuangalia maombi yaliyotolewa , kwamba
washtakiwa wote ni kosa lao la kwanza pia na aina ya makosa
yenyewe inawahukumu kutumikia kila mmoja kifungo cha
miaka 20 jela ….” Alihukumu .
Kwa mujibu wa hati mashtaka mahakamni
hapo watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo Februari 15,2013
mchana katika kijiji cha Msia kilichopo katika Bonde la Ziwa
Rukwa wilayani Sumbawanga.
Upande wa Mashtaka ulioongozwa na
Mwanasheria wa Serikali,Fadhili Mwandolo uliwaita mashahidi 12 akiwemo
mama mzazi wa mtoto Mwigulu,kwa sasa mtoto huyo anaishi nchini
Marekani .
Aidha kwa upande wa utetezi
uliokuwa na mawakili Baltazar Chambi,Charles Kasuku,Peter Kamyalile
na Mathia Budodi ulikuwa na mashahidi kumi .
Katika maombezi hayo
mawakili hao waliiomba mahakama iwaangalie washtakiwa hao kwa jino na
moyo wa huru kwa kuwa wamekaa mahabusu kwa miaka
minne na miezi minne .
Mwandishi:Petty Siame,Mhariri :Issack
Gerald
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments