Posts

POLISI,JAJI MKUU WATOA ONYO MGOMO WA MAWAKILI HAPA NCHINI-Agosti 28,2017

Image
Kaimu  Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Jeshi la Polisi nchini,wamelionya Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS),kutoingilia vyombo vya uchunguzi na upelelezi,vinavyochunguza tukio la mlipuko,uliotokea kwenye ofisi za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA usiku wa kuamkia juzi jijini Dar es Salaam.

POLISI WAWEKA WAZI MAJIBU YA UCHUNGUZI OFISI ZA MAWAKILI IMMMA KULIPULIWA-Agosti 28,2017

Image
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, leo limesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi yao walifika katika ofisi za Mawakili wa IMMMA Advocates wakiwa katika magari mawili na kujifanya ni maaskari na kuwarubuni walinzi na kuondoka nao katika gari mojawapo kabla ya kulipua jengo hilo.

RAIS MAGUFULI AWATAKA TAKUKURU KUTOKUWA NA KIGUGUMIZI DHIDI YA WAHUSIKA VITENDO VYA WA RUSHWA-Agosti 28,2017

Image
Rais Magufuli akiwa ndani ya Ofisi ya Takukulu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU ) kutokuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua pale wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

OFISI ZA WANASHERIA AKIWEMO MTOTO WA RAIS FATUMA KARUME NA LAURENCE MASHA ZATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO-Agosti 26,2017

Image
Sehenu ya majengo ya Ofisi Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya amethibitisha kushambuliwa ofisi za wanasheria za IMMMA saa 8 usiku wa kuamkia leo.

MANISPAA YA MPANDA YAPATA HATI SAFI UDHIBITI HESABU ZA SERIKALI,RC APONGEZA-Agosti 26,2017

Image
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Msaafu Raphael Mugoya Muhuga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral mstaafu Raphael Muhuga  ameipongeza halmashauri ya manispaa ya Mpanda kwa kupata hati nzuri  ya udhibiti wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka 2016.

HOFU JUU YA EBOLA YATANDA MKOANI RUKWA-Agosti 26,2017

Image
Kirusi cha Ebola WAKAZI mkoani Rukwa wametakiwa kuondoa hofu kutokana na kuwepo kwa taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa ebola baada ya mgonjwa mmoja kulazwa na kuendelea kupatiwa matibabu Katika hospital ya mkoa ya Sumbawanga anaeugua ugonjwa wenye dalili kama za homa ya Ebola.

RC RUKWA AZUIA UUZWAJI NJE MADINI YA CLINKER -Agosti 26,2017

Image
Bandari ya Kasanga RC-Rukwa-mbele-ya-Madini-ya-Clinker- Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amekamata na kuzuia uuzwaji wa tani 2,143 za madini aina ya “Clinker” yanayotumika katika kuzalishia saruji kutokana na wingu la ubabaishaji uliogubika usafirishaji wa madini hayo kwenda nje ya nchi hadi hapo atakapojiridhisha na utaratibu wa uuzwaji huo.