Posts

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YATENGA EKARI 2400 KWA AJILI YA UWEKEZAJI,SEKTA YA UFUGAJI,KILIMO,BIASHARA,UTALII,HUDUMA ZA JAMII NA MAKAZI YA WATU KUPEWA KIPAUMBELE-Agosti 21,2017

HALMASHAURI ya wilaya ya Mpanda mkoani katavi imesema  imetenga eneo la Luhafwe lenye ukubwa wa  ekari  2400  kwa ajili ya uwekezaji.

UGOMVI WA MKULIMA NA MFUGAJI WASABABISHA MAJERUHI KATAVI-Agosti 21,2017

WATU wawili wilayani Mpanda Mkoani Katavi wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao baada ya kuzuka ugomvi uliosababishwa na  kile kilichodaiwa ni kupishana kauli kati ya mkulima na mfugaji katika kijiji cha mbugani kata ya Kakese iliyopo manispaa ya Mpanda.

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA FUNGUZI WA MKUTANO WA 37 WA SADC MJINI PRETORIA-Agosti 19,2017

Image
Viongozi wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa  mkutano wa  37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mjini Pretoria, Afrika ya Kusini .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan leo amehudhuria  ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC mjini Pretoria Afrika Kusini akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli.

SERIKALI YA TANZANIA YASEMA UJIO WA NDEGE MPYA UKO PALEPALE-Agosti 19,2017

Image
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bibi. Zamaradi Kawawa  Serikali imethibitisha na kuwahakikishia Watanzania kuwa ujio wa ndege mpya ya tatu aina ya Bombardier Q400-Dash 8 upo pale pale licha ya baadhi ya wanasiasa wasio wazalendo kutumia kila njia kukwamisha ujio huo.

WANAFUNZI 22 WA SHULE YA SEKONDARI MIRAMBO MKOANI TABORA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUFANYA VURUGU-Agosti 19,2017

Image
JUMLA ya wanafunzi 22 wa shule ya sekondari Mirambo Mkoani Tabora,wamefikishwa na kusomewa mashtaka 12 yanayowakabili ikiwemo kufanya vurugu katika kata ya Chemchemi.

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI,WAMO WAWILI WA VYUO VIKUU,MWENYEKITI WA KAMPUNI YA KUHIFADHI MAFUTA,MWENYEKITI WA BARAZA LA USHINDANI -Agosti 18,2017

Image
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli,amefanya uteuzi wa viongozi mbali mbali akiwemo Mkuu wa chuo kikuu cha Ardhi.

MADAKTARI BINGWA KUTOKA DAE SES SALAAM WATOWEKA BILA TAARIFA KWA WAGONJWA MKOANI KATAVI,WAGONJWA WAHAHA KUPATA MATIBABU,MGANGA MKUU MKOA WA KATAVI ASHIKWA KIGUGUMIZI KUSEMA HALI ILIVYO-Agosti 18,2017

Image
Mh.Anna Lupembe Mbunge viti Maalumu Katavi(PICHA na.Issack Gerald) WAGONJWA ambao wamewasili  Mjini Mpanda wakitokea maeneo mbalimbali Mkoani Katavi kwa lengo la kupimwa na kutibiwa na madaktari bingwa wameeleza kusikitishwa na hatua ya madaktari hao kuondoka ghafla bila kutoa taarifa hatua ambayo imesababisha wagonjwa kupoteza muda na gharama za usafiri.