Posts

MANISPAA YA MPANDA YATOA MAJIBU KUHUSU WAKAZI WA MSASANI WATAKAOBOMOLEWA MAKAZI YAO : WASIO NA UWEZO WATAPEWA VIWANJA MTAA WA KAMPUNI,WENYE UWEZO KIASI WATALIPA KIDOGOKIDOO VIWANJA VILIVYOPIMWA-Julai 27,2017

HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imetenga viwanja vilivyopo katika mtaa wa Kampuni Kata ya Misunkumilo kwa ajili ya wakazi wa Mtaa wa Msasani watakaobomolewa makazi yao ambapo pia imesema watakaohitaji kupata viwanja vilivyopimwa ndani ya Manispaa watalazimika kulipa nusu ya gharama na kiasi kingine kulipwa baadaye.

KATIBU TAWALA WILAYA YA MPANDA AWAAGIZA MADIWANI MANISPAA YA MPANDA KUWASHIRIKISHA WANANCHI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA TAARIFA ZAO ZA USHIRIKI ZIWEKWE WAZI-Julai 27,2017

KATIBU tawala Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Sostenesi Mayoka,amewaagiza madiwani wa Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda kuwashirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo na kuonesha taarifa sahihi za ushiriki wao katika taarifa zinazoandaliwa.

PIKIPIKI YAGONGA GARI MKOANI KATAVI,WATU 2 AKIWEMO DEREVA NA ABIRIA WAKE WANUSURIKA KIFO-Julai 27,2017

WATU wawili akiwemo dereva wa piki piki maarufu kama boda boda akiwa abiria wake,wamenusurika kifo baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kugonga gari.

MKOANI KIGOMA MWENGE WA UHURU LEO UMEZINDUA MAJENGO YA KIBIASHARA NA MAJENGO YA KUKATIA TIKETI ZA MABASI-Julai 26,2017

MRADI wa majengo ya biashara  na vibanda vya  Kukatia tiketi Mkoani Kigoma umeziduliwa leo na mbio za mwenge katika stendi kuu ya mabasi iliyopo kata ya Gungu.

SERIKALI YA MTAA WA MPANDA HOTELI YAANZA KUCHUKUA HATUA WANAOKIUKA MASHARTI YA VIBALI VYA KUFYATUA TOFALI-Julai 26,2017

SERIKALI ya mtaa wa Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imeanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wanaokiuka masharti ya vibali halali walivyopewa kwa ajili ya kufyatua matofali katika mtaa huo.

PRF.LIPUMBA AWAVUA UANACHAMA WABUNGE 8 WA CUF NA MADIWANI 2-Julai 25,2017

Image
Profesa Lipumba Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) limewavua uanachama wabunge wanane wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu ikiwa ni pamoja na kukisaliti chama hicho.

RAIS MAGUFULI AHITIMISHA ZIARA YA SIKU 7 MIKOA YA KIGOMA,TABORA,KAGERA NA SINGIDA,YAFAHAMU YALIYOJILI KATIKA ZIARA HIYO-Julai 25,2017

Image
Rais wa Tanzania John Magufuli akizungmza na wananchi wa Singida Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Julai, 2017 amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku 7 katika Mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na Singida kwa kufungua barabara ya Itigi – Manyoni Mkoani Singida.