Posts

MABEHEWA YA MIZIGO TRENI YA TABORA–MPANDA YADONDOKA,WASAFIRI WANAOSAFIRI KUTOKA MPANDA-TABORA WAKWAMA WAENDELEA KUSOTA-Julai 24,2017

Image
Mwonekano wa treni ya Mpansa-Tabora(PICHA NA.Issack Gerald) WASAFIRI wanaotumia usafiri wa Treni kutoka Mpanda kuelekea Tabora wamekwama kuondoka tangu jana kwa kile kinachoelezwa kuwa mabehewa ya mizigo yameanguka. Wasafiri hao wakiwemo Grace Ndaiso,Marco Peter na Ester Abel wakizungumza na Mpanda Radio katika kituo cha Treni Mpanda wamesema,mpaka sasa hawana taarifa rasmi ya safari yao huku wasafiri wasiokuwa na pesa ya ziada wakipata adha ya njaa. Hata hivyo uongozi wa Treni kituo cha Mpanda haukuwa tayari kuzungumza na Mpanda Radio kuhusu mkwamo wa safari ya Treni,zaidi ya kusema wanaotakiwa kutoa taarifa ya kinachoendelea kuhusu safari hiyo ni uongozi wa kituo cha Treni upande wa Tabora kwa kuwa mabehewa ya mzigo yameangukia upande wa mkoa huo. Kauli kutoka kwa Mkuu wa kituo cha Treni Mpanda ambaye hakujitambulisha jina lake wakati akizungumza na Mpanda Radio ili kupata taarifa za kina kuhusu ajali hiyo iliyotokea jana,amesema hata yeye anawatafuta kwenye simu vi...

JESHI LA POLISI WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI LATAKA ULINZI NA USALAMA UANZIE KATIKA FAMILIA-Julai 23,2017

JESHI la polisi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,limewataka wananchi kuhakikisha ulinzi na usalama vinaanzia katika familia.

MKOANI KATAVI ELIMU KUHUSU RUSHWA YAHITAJIKA ZAIDI-Julai 23,2017

Image
VIONGOZI  wametakiwa kuisaidia jamii kujua umuhimu wa kutoa taarifa pindi  vitendo vya utoaji wa rushwa vinapotokea.

KATA YA MPANDA HOTEL ILIYOPO MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI KUTUMIA SHILINGI MILIONI 21.1 KUMALIZA TATIZO LA MAJI KATIKA MITAA YAKE-Julai 22,2017

KATA ya Mpanda Hotel iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imepata shilingi milioni 21.1 kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la maji ambalo limeikumba kata hiyo kwa muda mrefu.

MKUU WA WILAYA YA MPANDA LILIAN MATINGA AMWAGIZA MKURUGENZI MTENDAJI MANISPAA YA MPANDA KUTAFUTA VIWANJA KWA AJILI YA WAKAZI WA MTAA WA MSASANI KABLA YA BOMOA BOMOA-Julai 21,207

Image
MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Matinga,amemwangiza Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,kutafuta viwanja kwa ajili ya wakazi wa Mtaa wa Msaani kata ya Mpanda Hotel watakaobomolewa makazi yao kabla ya miezi sita waliyopewa kwisha. Katika picha kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda B.Lilian Charles Matinga(Picha na .Issack Gerald)

WAMILIKI VITUO VYA MAFUTA KATAVI,WAUNGA MKONO TAMKO LA RAIS MAGUFULI KUHUSU MASHINE ZA KIELEKTRONIKS-Julai 21,2017

Image
BAADHI ya wamiliki wa vituo vya mafuta vilivyopo Mkoani Katavi wameunga mkono tamko la Rais linalowataka kufunga mashine zinazotoa risiti za kielekroniks Bw.Malick Saidi ambaye ni Meneja kwa kampuni ya Mafuta ya GBP,kwa upande wake amesema mfumo huo utawaokolea muda pamoja na kampuni yake kukusanya mapato yote kama inavyotakiwa. Aidha Bw.Saidi akatoa ushauri kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoani Katavi kutokana na mfumo wa mashine za kielektroniks Wiki iliyopita,zaidi ya vituo vya mafuta 700 kote nchini vikiwemo vitano vilivyopo Mkoani Katavi vilifungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa madai ya kuikosesha serikali mapato kutokana na kutotumia mashine za kielektroniks EFD. Rais John Magufuli juzi akiwa Mkoani Kagera,ametoa siku 14 kwa makampuni ya mafuta nchini kuhakikisha wanafunga mashine hizo kinyume na hapo kampuni ambayo haitatekeleza agizo hilo Rais ameagiza ifungiwe na kunyang’anywa leseni ya Biashara. Muuzaji na mnunuzi wote wanajikuta hatiani kwa kukiuka ...

MKOA WA KATAVI WAFAULISHA MWANAFUNZI KATI YA KUMI BORA KITAIFA KIDATO CHA SITA 2017-Julai 21,2017

Image
JUMLA ya wanafunzi 574 kati ya 588 waliofanya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2017 mkoani Katavi wamefaulu huo ambapo Penina Mwalingo wa shule ya sekondari Mpanda Girls akishika nafasi ya 9 kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa waliofanya vizuri. Afisa Elimu wa Mkoa Katavi Mwalimu Godfrey Kalulu amesema Ufaulu kwa shule za Sekondari za kidato cha sita mkoani Katavi umeongezeka kwa asilimia 3.5 ambapo kwa mwaka 2017 ufaulu ni asilimia 69.5 ukitofautisha na asilimia 66.0 ya mwaka 2016. Katika picha ni Baadhi ya wanafunzi katika Shule ya Sekondari Mpanda Ndogo(PICHA NA Issack Gerald) Kalulu amesema shule ya Sekondari Karema imeshika nafasi ya kwanza Mkoani Katavi huku kitaifa ikishika nafasi ya 50 kati ya 449.