Posts

MKUU WA WILAYA YA MPANDA AHAMASISHA HARAMBEE KUWACHANGIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama- Mpanda Katavi MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi. Lilian Charles Matinga,ametoa wito kwa wakazi wa Wilaya ya Mpanda kujitokeza kwa hiari katika harambee ya kuwachangia wakazi wa Mkoa wa Kagera walioathiriwa wa tetemeko la ardhi Septyemba 10 mwaka huu.

KAMATI TENDAJI MRADI ELIMU JUMUISHI MKOANI KATAVI NA UJUMBE WA UGENI KUTOKA MIKOANI WAFANYA KIKAO KUJADILI MAHITAJI YA WATOTO WENYE ULEMAVU

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Katavi JAMII Mkoani Katavi imetakiwa kushiriki ipasavyo kuwafichua watoto wenye Ulemavu ili wapatiwe elimu kama watoto wengine wasio na ulemavu.

KUTOKA WILAYANI MLELE KATAVI -TUKIO LA NYUMBA KUCHOMWA MOTO

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama –Mlele Katavi NYUMBA za wakazi ambazo idadi yake haijafahamika eneo la Namba moja lililopo Kata na Tarafa ya Inyonga Wilayani Mlele Mkoani Katavi,leo zimeteketezwa kwa moto na baadhi ya mali zilizokuwemo kuteketezwa katika nyumba hizo. Kwa mjibu wa baadhi ya wakazi ambao mali zao zimeteketea ,wakizungumza na Mpanda Radio Kwa njia ya Simu kwa masikitiko makubwa akiwemo Bi.Tatu M asanja wamesema kuwa, tukio hilo ambalo wameliita la kushtukiza asubuhi ya leo,wamedai limetekelezwa na askari Mkoani Katavi kuanzia majira ya asubuhi. Wametaja baadhi ya mali zao ambazo zimechomwa kwa moto mbali na nyumba zao kuwa ni pamoja na Vyakula na mavazi huku watoto wakizagaa ovyo katika eneo hilo bila wazazi wao baada ya wazazi kukimbilia kusikojulikana kufuatia wengine kupigwa na askari hao. Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP damasi Nyanda,akizungumza na Mpanda Radio Kwa njia ya Simu mchana wa leo,amesema hajapata taarifa ya utekelezwaji wa...

KUHUSU SIKU YA AMANI DUNIANI,WAKAZI MKOANI KATAVI WASEMA HIKI

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Katavi BAADHI ya wakazi Mkoani Katavi,wameshauri siku ya amani duniani itumike kutafakari namna ya kudumisha amani iliyopo hapa nchini.                                   

TAASISI YA TWAWEZA WAENDESHA KONGAMANO LA WADAU WA ELIMU MPANDA,WAZAZI WALEZI WATAKIWA KUTAMBUA UMUHIMU WA ELIMU KWA WATOTO

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi WAZAZI na WALEZI katika manispaa ya Mpanda Mkoani wameshauri jamii kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto ikiwa ni urithi kwa maisha bora. Wanafunzi mkoani Katavi                                                

NYUMBA ILIYOTEKETEA KWA MOTO JUZI ,CHUMBA CHA MPANGAJI HASARA NI ZAIDI YA MILIONI MOJA NA LAKI TANO(1,500,000).

Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda Imebainika kuwa janga la moto lililotokea juzi katika Mtaa wa Mpadeco Kata ya Mkananyagio Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,umesababisha Bi.Grace Emmanuel Mkazi wa mtaa wa Mpadeco kata ya Makanyagio kupata hasara ya Zaidi ya Shilingi Miloni moja na laki tano (1,500 ,000). B.Grace amesema Moto huo uliozuka mchana uliunguza Vitanda 2 vyenye thamani ya laki tano na elfu sitini(560,000),Magodoro mawili 5 kwa 6 yenye thamani ya Shilingi laki tatu(300,000),Maguni ya Mpunga 4 thamani yake zaidi ya Shilingi laki 2(200,000),Upotevu wa fedha taslimu Shilingi laki nne na nusu za mkopo zilizopotea wakati wa uokozi na nguo ambazo tahamani yake haijafahamika. Akizungumza akiwa nyumbani kwake muda mfupi baada ya kutoka hospitali ya Wilaya ya Mpanda,alikolazwa baada ya kuzimia kutokana mshtuko alioupata baada ya kupata hasara hiyo,amesema kuwa hata hivyo hajatambua kiasi alichotumia kwa ajili ya matibabu. Hata hivyo amekwishafungua jarada Polisi ili ili kufany...

NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO MPANDA

Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda Moto umeunguza nyumba ya Familia moja na kusababisha hasara ya mali ambayo thamani yake haijajulikana katika mtaa wa Migazini kata ya Makanyagio   Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.