KAMATI TENDAJI MRADI ELIMU JUMUISHI MKOANI KATAVI NA UJUMBE WA UGENI KUTOKA MIKOANI WAFANYA KIKAO KUJADILI MAHITAJI YA WATOTO WENYE ULEMAVU
Na.Issack Gerald
Bathromeo Mashama-Katavi
JAMII Mkoani Katavi imetakiwa
kushiriki ipasavyo kuwafichua watoto wenye Ulemavu ili wapatiwe elimu kama
watoto wengine wasio na ulemavu.
Wito huo umetolewa leo na Verhan
Bakari ambaye ni mwezeshaji utathmini na utafiti wa mradi wa elimu Jumuishi kutoka chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru
Arusha ambaye amekuja Mkoani Katavi kutathmini
mafanikio na changamoto pia mikakati inayotakiwa kuchukuliwa ili kuendeleza mradi
wa elimu Jumuishi katika Mikoa ya Rukwa na Katavi.
Akizungumza na Kamati tendaji ya
kulea baraza la watoto wenye mahitaji maalumu Wilayani Mpanda katika Ofisi za
Kamati hiyo zilizopo Mpanda Mjini,Bw.Bakari amesema kila mtu kwa nafasi yake ni
wajibu wake kuhakikisha watoto wenye ulemavu hawanyanyapaliwi kwa namna yoyote hususani
katika sekta ya elimu au mahitaji ya msingi anayotakiwa kupatiwa.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa
elimu Jumuishi Mkoani Katavi Bw.Raphael Fortunatus,mbali na kutoa wito kwa
wazazi na walezi kuwapeleka shule watoto wenye uleamvu,amesema mafanikio ya
mradi huo ambayo yamepatikana kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 ni kuongezeka
wanafunzi walioandikishwa shuleni,ambapo kuanzia mwezi Januari 2016 mpaka mwezi
huu,zaidi ya watoto wenye ulemavu 90 wameandikishwa ikilinganishwa na watoto wapatao
50 waliokuwa wakiandikishwa kwa kipindi cha nyuma kabla ya mradi kuanza 2012.
Bw.Fortunatus ambaye pia ni Mwalimu
wa Shule ya Msingi Azimio anayefundisha wanafunzi wenye ulemavu,ametaja baadhi
ya maeneo ambayo wanafunzi wenye ulemavu wameongezeka kuandikishwa shuleni kuwa
ni pamoja na Kata ya Mwamkulu,Kakese na Manispaa ya Mpanda ambapo pia amesema kwa
sasa maeneo mengi yana majengo rafiki kwa mtoto mlemavu ikiwemo vyoo na madarasa.
Naye Serapioni Rwegasila ambaye ni
mzazi katika kamati ya kulea baraza la watoto Wilayani Mpanda,amesema bado kuna
wazazi na walezi hawatambui umuhimu wa mtoto mlemavu kupatiwa elimu na ameomba elimu
zaidi itolewe kwa wazazi hao wasiotambua umuhimu huo.
Mradi wa elimu Jumuishi ulioanza
mkoani Katavi mwaka 2012 unawezeshwa na Shirika la IFI lenye muunganiko wa
washirika watatu ambao ni Internation Aid Services(IAS),Free Pentecoastal
Church of Tanzania(FPCT) na International Centre Of Disability(CID).
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Mwandishi na Mhariri: Issack
Gerald Bathromeo Mashama
Comments