MKUU WA WILAYA YA MPANDA AHAMASISHA HARAMBEE KUWACHANGIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA
Na.Issack Gerald
Bathromeo Mashama- Mpanda Katavi
MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Charles Matinga,ametoa wito kwa wakazi wa Wilaya ya
Mpanda kujitokeza kwa hiari katika harambee ya kuwachangia wakazi wa Mkoa wa
Kagera walioathiriwa wa tetemeko la ardhi Septyemba 10 mwaka huu.
Mkuu
wa Wilaya Bi.Lilian ambaye pia ndiye mwenyekiti wa kamati ya maafa Wilayani
Mpanda,ametoa rai hiyo, wakati akizungumza na Mpanda Radio asubuhi ya leo
ambap[o amesema kuwa michango hiyo si lazima iwe fedha bali pia hata vitu kama
mabati,saruji na vifaa vingine vya ujenzi vinapokelewa.
Amesema
Mpaka sasa barua za harambee zimesambazwa kwa taasisi mbalimbali wilayani Mpanda
zaidi ya 68 ambapo pia wengine wenye moyo wa kuchangi wanaweza kuwasilisha
michango yao kupitia viongozi wa mitaa na vijiji pia kupitia kwa makatibu wa
kamati za maafa Wilaya ambao ni Wakurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya yaManispaa
ya Mpanda na Nsimbo.
Wakati
huo huo amesema kwa wakazi walio Nje ya Mpanda wanaruhusiwa kuchangia kupitia
namba za mitandao ya mawasiliano ambazo zimeambatanishwa katika barua za maombi
ya michango hiyo.
Katika
hatua nyingine amesema michango itakayokuwa imepatikana inatarajiwa kupokelewa
na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Raphael Mugoya Muhuga na hatimaye
kusalishwa kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.Kassim majaliwa ili michango hiyo
iwasilishwe Mkoani Kagera kwa wathirika.
Makumi
ya watu walipoteza maisha katika teemeko hilo huku mamia wakijeruhiwa na idadi
ya maelfu ya nyumba zikiharibiwa vibaya wakati huo huo shule na vituo vya
huduma za afya vikiharibiwa vibaya.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Mwandishi na Mhariri: Issack
Gerald Bathromeo Mashama
Comments