TAASISI YA TWAWEZA WAENDESHA KONGAMANO LA WADAU WA ELIMU MPANDA,WAZAZI WALEZI WATAKIWA KUTAMBUA UMUHIMU WA ELIMU KWA WATOTO
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
WAZAZI na WALEZI katika manispaa ya
Mpanda Mkoani wameshauri jamii kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto ikiwa ni
urithi kwa maisha bora.
Wanafunzi mkoani Katavi |
Ushauri huo umetolewa leo katika
kongamano la uwezo matokeo ya Elimu mwaka 2015, ambalo limewakutanisha wadau wa
elimu kujadili utafiti wa Uwezo-Twaweza na jinsi ya kutatua matatizo ya elimu.
Akizungumza wakati akifungua
kongamano hilo Mgeni rasmi ambaye ni Mdhibiti Ubora
wa shule,Mpanda mjini,Hartson Kyejo amesema,elimu ya msingi ndiyo
itakayomjengea uwezo mtoto kufanya vizuri maishani.
Wakizungumza
katika kongamano hilo,wadau wa elimu wamebainisha baadhi ya matatizo
yanayopelekea kudhorotesha elimu bora kwa wanafunzi wa shule za msingi kuwa ni
pamoja na watoto kuwa walezi wa watoto wenzao katika familia, upungufu wa
vyumba vya madarasa na utoro wa wanafunzi shuleni.
Kongamano
hilo limeandaliwa na Uwezo-Twaweza kwa kushirikiana na Katavi Women Development
Organization.
Katika Mkoa wa Katavi,Manispaa ya Mpanda ndiyo inayoongoza kwa namba moja kitaifa kwa miaka miwili mfululizo kwa kufaulisha mtihani wa darasa la saba ambapo ni mwaka 2014 na 2015 huku Mkoa wa Katavi kwa ujumla ukishika nafasi ya tatu kitaifa kwa kufaulisha wanafunzi.
Katika Mkoa wa Katavi,Manispaa ya Mpanda ndiyo inayoongoza kwa namba moja kitaifa kwa miaka miwili mfululizo kwa kufaulisha mtihani wa darasa la saba ambapo ni mwaka 2014 na 2015 huku Mkoa wa Katavi kwa ujumla ukishika nafasi ya tatu kitaifa kwa kufaulisha wanafunzi.
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri,tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Mwandishi : Tizibazomo Bernard
Mhariri :Issack
Gerald Bathromeo Mashama
Comments