KUHUSU SIKU YA AMANI DUNIANI,WAKAZI MKOANI KATAVI WASEMA HIKI
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Katavi
BAADHI ya wakazi Mkoani
Katavi,wameshauri siku ya amani duniani itumike kutafakari namna ya kudumisha
amani iliyopo hapa nchini.
Wakizungumza na Mpanda Radio
Fm,akiwemo Philbert John Mkazi wa kata ya Mpanda Hotel wamesema,amani
itadumishwa ikiwa kila mtu kila mtanzania ataheshimu sheria za nchi na kutambua
umhimu wa kuwa na amani hapa nchini.
Aidha wamesema,watanzania wanatakiwa kujifunza madhara yatokanayo na kukosekana kwa
amani kutoka nchini jirani zenye machaufuko zikiwemo Kongo na Burundi ambapo
miongoni mwa vyanzo vya uvunjifu wa amani ni mwenendo wa siasa.
Kwa mjibu
wa umoja wa mataifa siku hii imeandaliwa kipekee na baraza la Umoja wa Mataifa
kwa lengo la kuhakikisha dunia inakuwa mahali salama pa kuishi,kutokomeza
umaskini, kutokomeza vitendo vyote vya uvunjifu wa haki za binadamu na kukuza
mahusiano yanayoleta na kujenga amani.
Kwa mwaka
huu kitafa,maadhimisho hayo yamefanyika mkoani Dodoma na waandaaji wa siku hiyo
ni Umoja wa Mataifa kupitia kituo chake cha habari kwa kushirikiana na asasi
nyingine zisizo za kiserikali.
Siku ya
amani huadhimishwa Septemba 21 kila mwaka,ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu
inasema “Tokomeza Rushwa, Dumisha Amani”.
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri,tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Mwandishi : Issack
Gerald Bathromeo Mashama
Mhariri :Issack
Gerald Bathromeo Mashama
Comments