NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO MPANDA
Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
Moto
umeunguza nyumba ya Familia moja na kusababisha hasara ya mali ambayo thamani
yake haijajulikana katika mtaa wa Migazini kata ya Makanyagio Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Mashuhuda wa
tukio hilo Patrick Kapose na Elizabeth Matonge wamesema moto huo uliozuka
majira ya mchana umesababishwa na hitlafu ya umeme.
Aidha,kwa
mjibu wa mashuhuda,nyumba hiyo imeungua muda mfupi baada ya Shirika la Umeme
Nchini Tanesco Mjini Mpanda kufunga mita mpya baada ya kuondoa mita ya zamani
iliyokuwepo.
Kamanda wa
zimamoto aliyeongoza uzimaji wa moto huo amewataka wananchi kutoa taarifa
mapema mara tu majanga yanapotokea ili kuepusha athari zaidi.
Comments