VIJIJI ZAIDI YA 14 VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO KUPATA UMEME WA REA AWAMU YA III MWAKA 2016
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda,Katavi
Meneja wa
TANESCO mkoa wa Katavi Mhandisi Julius Sabu amesema katika awamu ya tatu ya
umeme wa REA wanampango wa kusambaza umeme katika vijiji ambavyo havikupitiwa
na mpango huo katika awamu zilizopita.
Meneja huyo
ametaja vijiji vitakavyonufaika na mradi wa REA wa awamu ya III kuwa ni Katumba,Mnyaki
A,Mnyaki B,Kaminula,Soko nne,Tambaza A,Tambaza B,Ivungwe A,Ivungwe
B,Nzanga,Iwimbi,Mtambo,Kalungu na Ndui Station.
Aidha Mhandisi
Sabu amesema kuwa tatizo la kukatika kwa umeme maeneo mbalimbali ya mji wa
mpanda inatokana na uchakavu wa mitambo ya kuzalisha nishati hiyo.
Kwa nyakati
tofauti ,wakazi wa Tarafa ya Katumba kwa
iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wilayani Mpanda Mkoani Katavi kwa
Ujumla wamekuwa wamelalamikia hali ya kukosekana kwa huduma ya nishati ya umeme
katika eneo lao.
Hata
hivyo,kumekuwa na tatizo la kukati kakatika kwa Umeme Wilayani Mpanda kwa
wakazi wa Mpanda Mjini wanaotengemea umeme wa Tanesco na hivyo kuathirika
kiuchumi ikizingatiwa kuwa mbali na kuunguliwa kwa vifaa vya ndani pia,wakazi
wengi wanakwama kuendesha biashara zinazotegemea umeme kama viwanda vya kukoboa
na kusaga nafaka.
Habari hii pia ipate
kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments