MKUU WA WILAYA TANGANYIKA:ENEO LA LUHAFE SASA KUJENGWA MJI WA MAKAZI NA BIASHARA.
Na.Issack Gerald Bathromeo
Mashama-Tanganyika
MKUU wa Wilaya ya Tanganyika
Bw.Salehe Mbwana Mhando,ametangaza wakazi wa eneo la Luhafe lililopo kata ya
Majalila,kulitumia eneo hilo kwa makazi na shughuli za kibiashara baada ya
mgogoro wa uhalali wa eneo hilo wa muda mrefu.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Saleh Mbwana Mhando akihutubia wakazi wa kitongoji cha Luhafe(PICHA NA.Issack Gerald)Septemba 16,2016 |
Mkuu wa Wilaya ametangaza uamuzi huo
jana,wakati akizungumza na wakazi wa eneo hilo ambao walitakiwa kuondoka tangu mwaka 2013 wakidaiwa kuvamia eneo hilo lililokuwa
limetengwa kwa ajili ya uwekezaji.
Aidha
Mkuu wa Wilaya amewataka wakazi wote waliovamia katika maeneo ya vyanzo vya
maji kujiondoa wenye kabla ya Oparesheni ya kuwaondoa kwa nguvu mwezi ujao wa
Oktoba mwaka huu ambapo miongoni mwa wanaotakiwa kutoweka na kusogea eneo la
Luhafe ni pamoja na waliopo eneo la Ijamba palipo na mto Sabaga,Western,Misanga
na Bariadi.
Kwa mjibu
wa taarifa ya kitongoji hicho ambayo imesomwa kwa mkuu wa Wilaya,eneo la Luhafe
lina wakazi wapatao elfu tatu wanaofanya shughuli ya kilimo na ufugaji.
Kwa
Upande wake Afisa Mipango miji na Vijiji katika Halmshauri ya Wilaya ya
Tanganyika Bw.Elisha Mengele,ametoa wito kwa uongozi wa eneo la Luhafe
kuendesha sensa ya kubaini idadi ya watu ili viwanja vipimwe na hatimaye kuanza
kujenga makazi ya kudumu baada ya kushidwa kufanya hivyo wakihofia kufukuzwa.
Naye
Filbert Kombe Nguvumali ambaye ni afisa elimu taaluma Halmshauri ya Wilaya ya
Tanganyika,amesema kwa sasa mpango uliopo ni kujenga shule za kudumu kwa ajili
ya wanafunzi wapatao zaidi ya 931 kuanzia chekechea hadi darasa la sita waliopo
katika vituo vinavyotumika kufundisha wanafunzi ambapo vituo hivyo vilikuwa
havitambuliki kwa serikali.
Hata
hivyo wakazi hao walidai kuwa mwaka 2013 walichomewa nyumba zao na mali
zilizokuwemo wakati wa uendeshaji wa Oparesheni Tokomeza ujangili.
Kwa
upande wao wananchi wamepokea kwa furaha tangazo la serikali kuwaruhusu kuishi
mahali hapo wakati mipango miji ikifanyika na hatimaye kuendesha shughuli za
biashara bila kikwazo.
Habari
hii pia ipate kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni
au ushauri au ukiwa na habari yoyote tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Comments