Posts

NAIBU WAZIRI JAFO AZINDUA MRADI WA MAJI NSIMBO WILAYANI MLELE

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi Naibu  Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi), Mh.Selemani Jafo akiwa na mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Nsimbo  Richard Mbogo amezindua mradi mkubwa wa maji Katika kijiji cha mwenge.                                                 

KATIBU TAWALA MKOA WA KATAVI AAGIZWA KUUNDA TUME YA KUCHUNGUZA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA KUMHUSU AFISA MIPANGO MANISPAA YA MPANDA

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi Naibu Waziri Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wakandarasi wanaojenga stendi ya mabasi mpanda. (PICHA NA.Issack Gerald) NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi),Selemani Jafo ameendelea na ziara yake leo mkoani Katavi ambapo amemuagiza Afisa Tawala wa Mkoa wa Katavi kuunda timu ya uchunguzi ili  kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka kwa Afisa Mipango miji wa Manispaa ya Mpanda ambapo anatuhumiwa kuchukua maeneo ya wananchi bila utaratibu. Naibu Waziri Suleiman Jafo akiwa na walimu wa shule ya sekondari Kabunga(PICHA NA.Issack Gerald)                                               

MCHUNGAJI MORAVIAN JELA MIAKA 20 KWA MENO YA TEMBO

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi MAHAKAMA ya Mkoa wa Katavi imemhukumu Mchungaji wa Kanisa la Moravian kijijini Usevya wilayani Mlele, Godwel Siame, kifungo cha miaka 20 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la uhujumu uchumi la kukutwa na meno ya tembo ya uzito wa kilo 20 yenye thamani ya Sh milioni 90. Meno ya Tembo                                                       

TRA RUKWA,KATAVI,MBEYA,SONGWE,RUVUMA NA IRINGA WATAKIWA KUIMARISHA KITENGO CHA TAHMINI KODI ISIYOMGANDAMIZA MFANYABISHARA

Na.Ofisi ya mwasiliano ya Waziri Mkuu  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa imeitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania kuimarisha kitengo cha tathmini ili kuweka viwango halali ambavyo havitawagandamiza wafanyabiashara na uwepo uwazi kuhusu viwango stahili vya kodi wanavyotakiwa kulipa.

BREAKING NEWS:SERIKALI YA WILAYA YA TANGANYIKA YAOMBA RADHI MAMA MJAMZITO KUJIFUNGULIA NJE AKIWA MBELE ZAHANATI IKIWA IMEFUNGWA

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika Serakali ya wilaya ya Tanganyika imeomba radhi wakazi wa kijiji na kata ya Ipwaga kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kwa kitendo cha mama mjamzito kujifungulia nje akiwa mbele ya zahanati baada ya kufikishwa kituoni hapo kutokana na kituo hicho kufungwa na muuguzi akiwa hayupo.                                            Zahanati ya Ipwaga ambayo mama mjamzito alijifungulia nje baada ya kufikishwa hapo(PICHA.Issack Gerald)

UNHCR WATOA MSAADA WA GARI LA MILIONI 78,732,000 KITUO CHA AFYA MISHAMO,WANANCHI HALMSHAURI WATAKIWA KULITUNZA NA KULITUMIA KATIKA MALENGO HUSIKA

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Shirika la kimataifa linalojishughulisha na kusaidia wakimbizi duniani UNHCR,limetoa msaada wa gari la wagonjwa kwa kituo cha afya cha Mishamo kilichopo kata ya Mishamo tarafa ya Mishamo Wilaya Mpya ya Tanganyika Mkoani Katavi. Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando akiwasalimia wagonjwa katika kituo cha afya cha Mishamo(PICHA NA.Issack Gerald)Agosti 5,2016 Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando mwenye suti nyeusi akizungumza na (katikati) ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Mishamo.Mkuu wa kituo Polisi Mishamo anaitwaOCS Ispecta MatongoMashaka na aliye kulia ni Afisa wa upelelezi Wilaya ya Tanganyika(PICHA NAIssack Gerald)Agosti 5,2016 Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando akitoka ndani ya Kituo cha afya Mishamo kusalimia wagonjwa(PICHA NAIssack Gerald)Agosti 5,2016                                    

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AFUTA RASMI USHURU,YEYE NA MKURUGENZI WA HALMSHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA WAACHA NAMBA ZA SIMU KWA WANANCHI ILI WAPOKEE KERO ZA WANANCHI HATA KWA SIMU

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Tanganyika  Saleh Mbwana Mhando ametangaza rasmi kufuta ushuru kwa fanyabiashara wadogo kwa wakazi wa Wilaya ya Tanganyika kama Rais wa Jamhuri ya Muungano alivyoagiza kufuta ushuru unaomkandamiza mwananchi. Baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Ipwaga wakimpokea Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando mara baadha ya kuwasili kijiji cha Ipwaaga(PICHA NA.Issack Gerald)Agosti 5,2016 Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando akisaini katika kitabu cha wageni Kijiji Ipwaga(PICHA NA.Issack Gerald)Agost  5,2016