UNHCR WATOA MSAADA WA GARI LA MILIONI 78,732,000 KITUO CHA AFYA MISHAMO,WANANCHI HALMSHAURI WATAKIWA KULITUNZA NA KULITUMIA KATIKA MALENGO HUSIKA
Na.Issack
Gerald Bathromeo
Shirika la kimataifa linalojishughulisha na kusaidia wakimbizi duniani
UNHCR,limetoa msaada wa gari la wagonjwa kwa kituo cha afya cha Mishamo
kilichopo kata ya Mishamo tarafa ya Mishamo Wilaya Mpya ya Tanganyika Mkoani
Katavi.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando akiwasalimia wagonjwa katika kituo cha afya cha Mishamo(PICHA NA.Issack Gerald)Agosti 5,2016 |
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando akitoka ndani ya Kituo cha afya Mishamo kusalimia wagonjwa(PICHA NAIssack Gerald)Agosti 5,2016 |
Akikabidhi gari hilo katika kituo cha
afya cha Mishamo kwa niaba ya UNHCR,Wakili wa UNHCR kituo cha makazi mapya kwa
watanzaia wapya waliokuwa wakimbizi Bw,Adolph Bishanga amesema gari hilo lenye
thamani ya shilingi Milioni 78,732,000 limetolewa katika kituo hicho ili kuunga
mkono serikali ya awamu ya tano ya kusaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa
gari la wagonjwa katika kituo hicho cha afya.
Aidha ametoa rai kwa wananchi
kilitunza vizuri huku akitaka Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika kutobadirisha
matumizi ya gari hilo na badala yake litumike kwa matukio ya dharula hususani
kwa wakazi wa Mishamo.
Amesema gari la awali lambalo lilitolewa
na UNHCR mwaka 2012 mpaka sasa halijulikani lilipo baada ya Halmshauri
kubadirisha kituo inapotakiwa kutoa huduma gari ambalo halikujulikana lilipo
miezi mitatu tangu kukabidhiwa.
Bw.Bishanga amesema kuwa UNHCR
litaendelea kushrikiana na serikali ya Tanzania kutatua changamoto mbalimbali
hususani katika sekta ya Afya na elimu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando akipokea gari hilo na kulikabidhi kwa
wananchi kupitia kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw.Ngalinda Hawamu Ahmada mbabli na
kulipongeza Shirika la UNHCR kwa msaada huo,ametaka pia wananchi wa Mishamo na
Wilaya ya Tanganyika kwa ujumla kulitunza vizuri gari hilo.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw.Ngalinda
Hawamu Ahmada ametoa onyo kwa mtumishi yeyote kutotumia gari hilo kama daladala
katika shughuli binafsi na atakayefanya hivyo atashughulikiwa kwa mjibu wa
kanuni na taratibu.
Wakazi wa Kata ya Mishamo na wakazi
wengine wote wanaotegemea kupata huduma ya gari hilo na katika kituo cha afya
mishamo wamepongeza hatu ya UNHCR kutambu uhai na thamani ya wakazi wa Mishamo.
Katika ziara ya mkuu wa Wilaa
aliyoifanya jana,aliambatana pia na wakuu wa idara mbalimbali wa afya wakiwemo
Kaimu mganga mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Dkt.Mhamed Mpunjo na Muuguzi Mkuu
Wilaya ya Tanganyika.
Mhariri:Issack
Gerald Bathromeo
Habarika Zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPO.COM
Comments