MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AFUTA RASMI USHURU,YEYE NA MKURUGENZI WA HALMSHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA WAACHA NAMBA ZA SIMU KWA WANANCHI ILI WAPOKEE KERO ZA WANANCHI HATA KWA SIMU
Na.Issack Gerald Bathromeo
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Tanganyika Saleh Mbwana Mhando ametangaza rasmi kufuta ushuru kwa
fanyabiashara wadogo kwa wakazi wa Wilaya ya Tanganyika kama Rais wa Jamhuri ya
Muungano alivyoagiza kufuta ushuru unaomkandamiza mwananchi.
Baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Ipwaga wakimpokea Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando mara baadha ya kuwasili kijiji cha Ipwaaga(PICHA NA.Issack Gerald)Agosti 5,2016 |
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando akisaini katika kitabu cha wageni Kijiji Ipwaga(PICHA NA.Issack Gerald)Agost 5,2016 |
Bw.Mhando ametangaza jana rasmi
kufuta ushuru huo wakati akizungumza na
wakazi wa kata za Ipwaga na Mishamo alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa
wananchi na kusikiliza kero za wananchi wa kata hizo.
Amesema kuwa,wanaotakiwa kulipa
ushuru ni wafanyabiashara wanaosafirisha mizigo kutoka sehemu moja kwenda
sehemu nyingine kwa ajili ya baiasahara na siyo mkulima wa kawaida anayetoa
mazao shambani kwenda kula au muuzaji wa bidhaa ndogondogo kama vile
nyanya,mchicha,dagaa na bidhaa nyingine ndogondogo kwa ajili ya kujikimu kimaisha.
Aidha amesema kuwa mtoza ushuru wa
aina yoyote aliyekuwa akitoza ushuru ni bora akafanye kazi nyingine ili
kujiepusha kujiweka katika matatizo kwa serikali ya awamu ya tano imelenga
kumsaidia mwananchi wa hali ya chini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji
Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika amesema ni wakati wa kutenda kuliko maneno
kwa kuwa wananchi wanahitaji maendeleo na kusisitiza kuwa serikali haitamfumbia
macho mtumishi wa Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika atakayekiuka kanuni za
utumishi na maadili ya kazi yake anayotakiwa kuitekeleza.
Kwa upande wao wakazi wa kata za Mishamo na Ipwaga wakizungumza kwa furaha,wamepongeza Serikali ya
Wilaya ya Tnaganyika na serikali ya awamu ya tano kwa kufuta ushuru
unaomkandamiza mwananchi na kusema kweli serikali ya awamu ya tano imelenga
kuwakomboa.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya
Wilaya ya Tanganyika Bw.Ngalinda
Hawamu Ahmada wamewaachia namba za simu wananchi ili wazitumie kuwa pigia
wanapoona kuna kero katika maeneo yao ikiwemo kero za viongozi wao
kuwanyanyasa,kutopata huduma za jamii ipasavyo kama hospitalini na watendaji
wote watakaotenda kinyume na kanuni za utumishi.
Hata hivyo wamesisitiza kutotumia
namba hizo kuongea majungu isipokuwa watoe taarifa zenye ukweli ili zidfanyiwe
kazi haraka na mwananchi yeyote atakayetoa taarifa za uongo pia naye
atashughulikiwa kisheria.
Mhariri:Issack
Gerald Bathromeo
Habarika Zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPO.COM
Comments