MCHUNGAJI MORAVIAN JELA MIAKA 20 KWA MENO YA TEMBO
Na.Issack Gerald
Bathromeo-Katavi
MAHAKAMA ya Mkoa wa Katavi imemhukumu Mchungaji wa Kanisa la
Moravian kijijini Usevya wilayani Mlele, Godwel Siame, kifungo cha miaka 20
jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la uhujumu uchumi la kukutwa na meno ya
tembo ya uzito wa kilo 20 yenye thamani ya Sh milioni 90.
Meno ya Tembo
Hakimu wa Mahakama hiyo,Mh.Chiganga Tengwa akisoma hukumu
hiyo jana alisema ameridhishwa na ushahidi usiotia shaka yoyote uliotolewa na
upande wa mashitaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.
“Nimelazimika kutoa adhabu kali ili iwe fundisho sio kwa
mshtakiwa tu, bali kwa wengine wenye tabia kama yake,” alisisitiza.
Kwa upande wa mashtaka uliita mashahidi sita huku upande wa
utetezi ukiongozwa na Wakili wa Kujitegemea,Patrick Mwakyusa uliita mashahidi
wanne mahakamani hapo.
Awali,Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali Mfawidhi,
Achiles Mulisa alieleza mahakamani hapo kwamba mshtakiwa alitenda kosa hilo Mei
5, mwaka huu.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio, mshtakiwa alikutwa na nyara
hizo za serikali zenye uzito wa kilo 20 zikiwa na thamani ya Sh milioni 90
zikiwa zimefichwa katika ofisi ya mshtakiwa katika Kanisa la Moravian kijijini
Usevya.
Akijitetea, mshtakiwa aliomba mahakama hiyo impunguzie adhabu
kwamba lilikuwa kosa lake la kwanza huku akisisitiza kuwa alikuwa hafahamu
nyara hizo za serikali zilifikishwaje ofisini kwake kwenye kanisa hilo.
Endeleo kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Meno ya Tembo |
Comments