KATIBU TAWALA MKOA WA KATAVI AAGIZWA KUUNDA TUME YA KUCHUNGUZA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA KUMHUSU AFISA MIPANGO MANISPAA YA MPANDA
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
Naibu Waziri Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wakandarasi wanaojenga stendi ya mabasi mpanda.(PICHA NA.Issack Gerald) |
Naibu Waziri Suleiman Jafo akiwa na walimu wa shule ya sekondari Kabunga(PICHA NA.Issack Gerald) |
Jafo
katika ziara hiyo ametembelea wilaya ya Tanganyika na wilaya ya Mpanda.
Katika
wilaya ya Tanganyika aliambatana na Mbunge wa Jimbo la Mpanda vijijini Moshi
Kakoso ambapo alikagua mradi wa Maktaba ya shule ya sekondari Kabunga pamoja
na mradi wa Maji katika jimbo la mpanda vijiji.
Kwa
upande wa Manispaa ya Mpanda alifanikiwa kukagua hospitali ya wilaya ya Mpanda
pamoja na ujenzi wa stendi ya mabasi ya kisasa.
Hata
hivyo Jafo ilihitimisha kwa kufanya mkutano na watumishi wote wa Halmashauri ya
Mpanda pamoja na Manispaa ya Mpanda katika ukumbi wa idara ya maji uliopo
mjini Mpanda.
Naibu
Waziri ameendelea kutoa maelekezo ya utendaji kazi kwa watumishi wa serikali za
mitaa kwa kuzingatia dhana kubwa ya mabadiliko.
Katika
majumuisho hayo, Jafo hakufurahishwa na tabia ya baadhi ya watumishi wenye
tabia ya ubadhirifu wa fedha za umma na kutowajali wananchi.
Kuhusu
Afisa mipango huyo, Jafo amesema amewapa fedha kidogo wananchi wenye ardhi nje
ya utaratibu kisha kuyauza maeneo hayo kwa gharama kubwa kwa matajiri.
Kadhalika,
Jafo amesema Afisa huyo analalamikiwa kuhodhi viwanja kadhaa ndani ya Manispaa
hiyo kwa kutumia wadhifa alionao.
“Kutokana
na tuhuma hizo namuagiza Katibu tawala mkoa(RAS) Katavi kuunda timu ya
uchunguzi kisha kuwasilisha ripoti Ofisi ya Rais Tamisemi kwa hatua za
kinidhamu endapo itabainika ukweli wa tuhuma hizi,”alisema Jafo.
Endelea
kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments