NAIBU WAZIRI JAFO AZINDUA MRADI WA MAJI NSIMBO WILAYANI MLELE
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali
za Mitaa(Tamisemi), Mh.Selemani Jafo akiwa na mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la
Nsimbo Richard Mbogo amezindua mradi mkubwa wa maji Katika kijiji cha
mwenge.
Sambamba na uzinduzi huo pia ameweka jiwe la msingi katika
ujenzi wa madarasa mawili, vyoo na nyumba ya walimu Katika shule ya
sekondari Machimboni iliyopo katika halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi.
Baada ya uzinduzi wa miradi hiyo, Jafo amezungumza na
watumishi wa halmashauri hiyo kwa lengo la kukuza utendaji kazi wa watendaji wa
halmashauri hiyo ili kuongeza utoaji wa huduma kwa wananchi.
Endelea
kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments