BREAKING NEWS:SERIKALI YA WILAYA YA TANGANYIKA YAOMBA RADHI MAMA MJAMZITO KUJIFUNGULIA NJE AKIWA MBELE ZAHANATI IKIWA IMEFUNGWA
Na.Issack Gerald
Bathromeo-Tanganyika
Serakali ya wilaya ya Tanganyika
imeomba radhi wakazi wa kijiji na kata ya Ipwaga kilichopo Halmashauri ya
wilaya ya Tanganyika kwa kitendo cha mama mjamzito kujifungulia nje akiwa mbele
ya zahanati baada ya kufikishwa kituoni hapo kutokana na kituo hicho kufungwa
na muuguzi akiwa hayupo.
Zahanati ya Ipwaga ambayo mama mjamzito alijifungulia nje baada ya kufikishwa hapo(PICHA.Issack Gerald) |
Tamko la wananchi hao kuombwa radhi
na serikali limetolewa na mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Saleh Mbwana Mhando
kwa niaba ya serikali ya Wilaya ya Tnganyika wakati akizungumza na wakazi wa
kijiji na kata ya Ipwaga.
Amesema kuwa serikali imekiri kukosea
akisema kuwa muunguzi aliyekuwepo alikuwa amepeleka mafaili Hospitali ya Wilaya
Mpanda na zahanati kukosa mtu aliyetakiwa kuwepo na kupelekea tukio hilo
kutokea.
Taukio la mama kujifungulia nje ya
Zahanati lilitokea Agosti 1 mwaka huu likimhusisha mwanamke mjamzito
aliyetambulika kwa jina la Neema Sostene(31) kutoka kijiji cha Mwibasi.
Hata hivyo hatua ya Bw.Ngalinda
Ahmada ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika Kumpatia barua ya Onyo Muuguzi huyo
kilionekana kuwakwaza baadhi ya wananchi waliokuwepo katika mktano wakidai kuwa
ni vema serikali ndiyo ingewajibika na siyo kumwajibisha muuguzi huku
wakitambua kuwa yupo peke yake ambapo anatakiwa kufanya kazi mbalimbali
zikiwemo kupima wagonjwa,kutoa dawa kwa wagonjwa,kusaidia wanawake wajawazito
wanaotaka kujifungua na kufanya kazi za kiofisi.
Wakati huo huo zahanti hiyo imeongezewa muuguzi mwingine ili
kusaidia huduma mbalimbali katika zahanati hiyo ikiwemo kusaidia akina mama
wajawazito wenye uhitaji wa kujifungua ambapo muuguzi huyo ametolewa katika
kituo cha afya Mishamo.
Wengine ambao Mkurugenzi alisema
lazima wawajibishwe ni Maafisa watendaji wa kijiji na kata na Diwani kwa kutotoa taarifa katika
mamlaka husika mpaka Mkurugenzi mwenyewe alipopata taarifa kutoka kwa raia.
Kwa upande wake Muuguzi huyo
aliyepewa onyo,amekiri kutokuwepo katika zahanati akidai kuwa alikuwa amepeleka
nyaraka Mpanda Mjini alizokuwa ameagizwa na Viongozi wake aziwasilishe ambapo
hata hivyo amekanusha taarifa zilizotangazwa na Shirika la Utangazaji TBC kuwa
hakuwepo katika kituo cha kazi kwa siku nyingi.
Hata hivyo zahanati hiyo bado in
changamoto ya upungufu wa vitanda vya kujifungulia wajawazito.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habrika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments