TRA RUKWA,KATAVI,MBEYA,SONGWE,RUVUMA NA IRINGA WATAKIWA KUIMARISHA KITENGO CHA TAHMINI KODI ISIYOMGANDAMIZA MFANYABISHARA
Na.Ofisi ya mwasiliano ya Waziri Mkuu
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa imeitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania kuimarisha kitengo cha
tathmini ili kuweka viwango halali ambavyo havitawagandamiza wafanyabiashara na
uwepo uwazi kuhusu viwango stahili vya kodi wanavyotakiwa kulipa.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni
(Jumapili, Agosti 07, 2016) wakati alipozungumza na viongozi wa mikoa ya Mbeya,
Katavi, Songwe, Rukwa, Ruvuma, Iringa na Njombe mara baada ya kuwasili mkoani
Mbeya kwa ajili ya kufunga maadhimisho ya maonyesho ya nane nane kwa mikoa ya
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika mkoani Mbeya.
Ili kufanikisha mpango huo Waziri Mkuu
amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuwasikiliza wafanyabiashara ambao wana
malalamiko ya kweli ya kutotendewa haki katika kutozwa kodi kwa sababu mchango
kupitia kodi ni kwa ajili ya kuendeleza uchumi wa Taifa.
Katika hatua nyingine ameitaka idara ya
Uhamiaji ijikite katika kudhibiti watumishi wasiokuwa waaminifu ambao wamekuwa wakichukua
rushwa kutoka kwa wageni wanaotoka nje ya nchi na kuwaingiza nchini bila ya
kuwa na vibali maalumu.
Alisema kitendo cha mipaka kushindwa
kudhibitiwa na kuruhusu uingiaji holela wa watu wasiokuwa na vibali chini
kunasababisha Serikali kushindwa kuteleza ipasavyo mipango yake ya kuwahudumia
wananchi kulingana na idadi halisi.
Mbali na kuiagiza Idara ya Uhamiaji pia
Waziri Mkuu alisema wakuu wa mikoa ya mipakani wana jukumu la ziada la
kuhakikisha wanadhibiti mipaka yote na kuhakikisha hakuna watu wanaoingia
nchini bila ya kuwa na vibali.
Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka wakuu wa
mikoa kote nchini kuendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo
yao na kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu ili Watanzania
waweze kutekeleza shughuli zao za maendeleo kama walivyojipangia.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Makalla
alipokuwa akisoma taarifa ya mkoa huo kwa Waziri Mkuu alisema mkoa huo una
jumla ya viwanda 1,653 kati yake vikubwa ni tisa, vya kati 19 na vidogo
1,625 na bado wanaendelea kuzisimamia halmashauri kutenga maeneo zaidi kwa
ajili ya kuongeza na kupanua viwanda.
Mhe. Makalla alisema katika eneo hilo la
viwanda mkoa una kiwanda kimoja cha kusindika nyama cha Tanganyika Pachers
kilichopo wilayani Mbeya ambacho hakijawahi kufanya kazi tangu kilipojengwa na
kufungwa mitambo mwaka 1975.
Mkuu huyo wa mkoa alisema usimamizi wa
kiwanda hicho uko chini ya Masajili wa Hazina na kwamba tayari kuna muwekezaji
amepatikana kwa ajili ya kukiendesha hivyo ameiomba Serikali kuharakisha
taratibu za mikataba ili kiweze kuanza kufanya kazi.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments