WAENDESHA pikipiki maarufu kama bodaboda mkoani Katavi,wameiomba serikali kuwapatia elimu ya udereva pamoja na kupatiwa mtambo wa kukata reseni za udereva ili kupunguza ajali za barabarani .
WANANCHI wa kijiji cha Kamilala kata ya Katuma tarafa ya Mwese wilayani Tanganyika mkoani Katavi,wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa shamba lililochukuliwa na mtu moja aliyefahamika kwa jina la Kiyondo zaidi ya ekari 1800 huku wananchi wakiwa hawana maeneo ya kulima .
Wakazi wa kata ya Itenka iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Wilayani Mlele Mkoani Katavi,wameiomba Serikali ya halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo kutatua changamoto za miundombinu ya barabara kuanzia Mpanda Mjini hadi Itenka.
CHAMA cha walimu CWT mkoani katavi kimesema kitahakikisha kinapigania maslahi ya walimu wanawake makazini kwa sababu ya mchango kubwa walionao katika jamii.
SHULE ya msingi kasekese iliyopo kata ya kasekese wilaya mpya ya Tanganyika mkoani katavi wametengewa fedha kiasi cha shillingi milion 52 kwa ajili ya kutatua changamoto ya vyumba vya madarasa. Kauli hiyo imetolewa na mbunge wa mpanda vijijini Mh.Suleman Kakoso baada ya kutembelea kijijini hapo kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa kumchagua. Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kasekese kata ya Kasekese(PICHA NA Issack Gerald)