EKARI 1800 ZAMILIKIWA NA MWANANCHI MMOJA,WANANCHI WAHAHA MAHALI PA KULIMA WAIOMBA SERIKALI WILAYANI TANGANYIKA KUINGILIA KATI.
WANANCHI wa
kijiji cha Kamilala kata ya Katuma
tarafa ya Mwese wilayani Tanganyika
mkoani Katavi,wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa shamba
lililochukuliwa na mtu moja
aliyefahamika kwa jina la Kiyondo zaidi ya ekari 1800 huku wananchi wakiwa
hawana maeneo ya kulima .
Wamesema
hayo wakati wakizungumza na Mpanda radio kijijini hapo,juu ya mgogoro
unaowakabili ambapo wameeleza kuwa hawana maeneo ya kulima .
Kwa upande
wa mwenyekiti wa kijiji cha kamilala Dady Stasheni Songoi amesema kuwa, Bw.Kiyondo amechukua eneo hilo la
wananchi bila kufuata utaratibu.
Kutokana na hatua hiyo wananchi waliamua kufyeka shamba hilo jambo ambalo likamlazimu Kaimu mtendaji ambaye pia ni mkuu
wa shule ya msingi Kayenze Bw.Donatusi
Sixmod kufika eneo la tukio na kuzungumza na wananchi hao,waliokuwa na
hasira kali huku akiwaomba kuwa na subira wakati jitihada zikiendelea
kufanyika.
Mwa ndishi:Ester Lameck
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea
kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments