WAWILI WAJINYONGA WILAYANI MPANDA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI
WATU wawili
Mkoani Katavi wamefariki dunia kwa nyakati
tofauti kwa kujinyonga.
Tarifa hiyo imetolewa
leo na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Damas Nyanda,wakati akizungumza
na Mpanda radio ofisini kwake juu ya matukio hayo.
Kamanda
Nyanda amewataja waliofariki kuwa ni Sumpuli Alikado mkazi wa mtaa wa zamani
kata ya kashaulili na Alex Charles mkazi wa Kilimahewa Kata ya Shanwe.
Mpaka sasa
chanzo cha vifo hivyo bado hakijulikani na upelelezi unaendelea kufanyika.
Matukio ya
watu kujinyonga Wilayani Mpanda na Katavi kwa ujumla yamekuwa yakitokea ikiwemo
Wilaya ya Mpanda.
Mwandishi:Ester Lameck
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments