MKUU WA WILAYA YA MLELE AJITAMBULISHA KWA WATUMISHI HALMASHAURI YA WILAYA YA MLELE
MKUU wa
wilaya ya mlele mkoani Katavi Bi.Recho Kasanda ametoa agizo kwa watumishi wa
wilaya hiyo kufanya kazi wa kuzingatia taratibu na sheria.
Kasanda
ametoa agizo hilo akiwa katika kikao cha
utambulisho kwa watumishi wa ofisi ya
mkuu wa wilaya na Halmashauri ya Wilaya ya
Mlele,shughuli iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Inyonga.
Sambamba na
hilo amewataka pia watumishi kusafirisha
nyaraka za serikali kwa njia sahihi,ili kuhakikisha usalama wa nyaraka husika
na utunzaji wa siri wa serikali kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kiutumishi.
Mwandishi:Ester Lameck
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments