BODABODA KATAVI WAOMBA ELIMU YA UDEREVA NA MTAMBO KWA KUKATA LESENI
WAENDESHA
pikipiki maarufu kama bodaboda mkoani Katavi,wameiomba serikali kuwapatia elimu
ya udereva pamoja na kupatiwa mtambo wa kukata reseni za udereva ili
kupunguza ajali za barabarani .
Kauli hiyo
imetolewa na mwanyekiti wa chama cha waendesha bodaboda Stephano Mwakabafu
alipokuwa akizungumzia mafanikio ya kuanzishwa kwa chama hicho ambacho
kimesaidia kupunguza ajari za
barabarani.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoani katavi Nasoro Alfi,amewataka wananchi kuonyesha
ushirikiano baina yao na madereva na kutoliachia suala la usalama jeshi la
polisi peke yake.
Aidha
amewaasa vijana wa stendi kufanya kazi
eneo walilopangiwa na endapo watabainika kukutwa eneo ambalo
hawajasajiliwa hatua za kisheria
zitachukuliwa.
Mwandishi:Ester Lameck
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments