SHULE ya
msingi kasekese iliyopo kata ya kasekese wilaya mpya ya Tanganyika mkoani
katavi wametengewa fedha kiasi cha shillingi milion 52 kwa ajili ya kutatua
changamoto ya vyumba vya madarasa.
Kauli hiyo
imetolewa na mbunge wa mpanda vijijini
Mh.Suleman Kakoso baada ya kutembelea
kijijini hapo kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa kumchagua.
|
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kasekese kata ya Kasekese(PICHA NA Issack Gerald) |
Aidha Kakoso amewashukuru wananchi hao kwa kujitolea kujenga baadhi ya vyumba vya
madarasa bila kuwepo kwa nguvu ya serikali ambapo amewaasa kutokata tamaa
katika kuboresha miondombinu ya elimu kwa ujumla.
Shule nyingi zilizopo vijijini
zinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa vinavyoendana na
idadi ya wanafunzi pia upungufu nyumba za walimu.
Mwa ndishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments