CWT KATAVI KUPIGANIA HAKI ZA WALIMU WANAWAKE
CHAMA cha
walimu CWT mkoani katavi kimesema kitahakikisha kinapigania maslahi ya walimu
wanawake makazini kwa sababu ya mchango kubwa walionao katika jamii.
Hayo
yamesemwa na katibu wa chama cha walimu mkoa wa katavi Bi.Lucy Masengenya katika
mkutano mkuu wa chama cha walimu uliojumuisha walimu wanawake kutoka maeneo
mbalimbali mkoani Katavi.
Aidha Bi. Masengenya amesema kuwa chama
kinatakiwa kuhakikisha kinapata viongozi wanawake wanaotoka ndania ya Chama cha
walimu wenye ujuzi wa kutosha mara baada ya kuwezeshwa katika haki zao.
Akizungumza
baada ya ufunguzi wa mkutano huo bi Masengenya
amesema ulinzi huo utaenda sanjari na kuondoa vikwazo vinavyowanyima haki na
fursa sawa na wanaume katika ajira na
mafunzo hatua ambayo imeungwa mkono na baadhi ya walimu.
Comments