CHANGAMOTO LUKUKI ZAENDELEA KUKWAMISHA MAENDELEO YA WANANCHI KATA YA ITENKA.
Wakazi wa kata ya Itenka iliyopo
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Wilayani Mlele Mkoani Katavi,wameiomba Serikali
ya halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo kutatua changamoto za miundombinu ya barabara
kuanzia Mpanda Mjini hadi Itenka.
Kwa muda mrefu wakazi wa kijiji na
kata ya Itenka eneo lililo kitovu cha uchumi wa Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo wamekuwa
wakisumbuliwa na changamoto lukuki zikiwemo za kutokuwepo kwa maji safi na
salama ambapo katika huduma ya wanalazimika kunywa maji ambayo yanakanyagwa na
watu wanapokuwa wanagombania maji hayo huku wanyama kama mbwa nao wakinywa maji
katika visima hivyo vifupi ambavyo vimechimbwa na wananchi hao katika kuonesha
jitihada za kutatua ukosefu wa maji.
Wakizungumza na Mpanda Radio kijijini
Itenka kwa hisia kali za maumivu ambayo yamesnbabishwa matatizo waliyonayo
kutokanana na kukosa huduma za jamii,wamesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya
Nsimbo,Wilaya ya Mlele na mkoa wa Katavi wamekuwa kama wameisahau kata ya
Itenka huku wananchi hao wakisisitiza kuwa kwa nafasi zao wako tayari kuchangia
kwa asilimia 20 wanazotakiwa kuchangia isipokuwa wamekwamishwa na mipango ya
serikali.
Changamoto nyingine ambazo zimetajwa
na wananchi hao kukosekana kwa kituo cha afya na ukosefu wa stendi ya Magari
ambapo mara kwa mara watu hunusurika kugongwa na magari hao sambamaba na
pikipiki kutokana na kutokuwa na sehemu maalumu ya kupaki vyombo hivyo vya
usafiri.
Wakitolea ufafanuzi kuhusu barabara
inayoanzia Mpanda Mjini hadi Itenka,wakazi hao wamesema kuwa barabara imekuwa
ikikwanguliwa na kuwekwa chanagalawe na changalawe kumomonyoka na kusambaa
kutokana na kuonekana kujengwa chini ya kiwango na kuwa shida wakati wa masika
ambapo mapaka sasa barabara yote imejaa mchanga hali inayopelekea magari na
pikipiki kushindwa kupita hususani barabara kutoka Itenka kuelekea vijiji vya
vya Imilamate na Mwamkalu.
Katika hatua nyingine wakazi wa
Itenka,wameiomba serikali kuondoa mageti mengi yaliyowekwa barabarani karibu na
mashamba yao ili kuwatoza ushuru kinyume na alivyoagiza Rais John Magufuli huku
wakitaka kutofautishwa kati ya mkulima anayetoa mazao shambani na mfanyabiashara
anayesafirisha mazao kwa ajili ya biashara.
Wamesema serikali inatakiwa kusimamia
agizo la Mkuu wa Nchi Rais Dkt.John Pombea Magufuli aliyeagiza kuondolewa
mageti yasiyo ya lazima barabarani yanayomnyonya mkulima na mfanyabiasahara
ambapo Rais magufuli aliagiza kuondolewa kwa vizuizi barabarabani ikiwa ni
kutekeleza ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015.
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo
Bw.Joseph Raulence Mpemba amekiri kuwepo kwa changamoto hizo lukuki katika kata
ya Itenka ambapo amesema kuwa katika sekta ya afya zimetengwa Shilingi milioni
70 kujenga kituo cha Afya kijijini Itenka kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Bw.Mpemba akizungumzia kuhusu kuwepo
kwa mageti mengi amesema kuwa geti linalotakiwa kuwepo ni moja tu na siyo zaidi
ya matano yaliyopo kwa sasa hali inayoleta utata kwa wakulima na
wafanyabiashara ambapo kwa sasa wanalazimika kuchangia zaidi ya mara moja
upande wa Nsimbo na Mpanda na kuendelea kujikita katika dimbwi la umaskini.
Aidha Bw.Mpemba amesema suala la maji
ni tatizo kubwa na amethibitisha ukubwa wa tatizo ambapo huenda muda wowote
magonjwa ya tumbo yakawakumba wakazi wa itenka kutokana na hali ya huduma ya
maji ilivyo kwa sasa ikiwa serikali haitaweka mkono wako na kutupia macho yake
kata hiyo.
Kata ya Itenka inasifika kwa shughuli
za kilimo huku zao kubwa linalozaliwa zaidi na kukuza uchumi wa Halmashauri na
Mkoa likiwa Mpunga ambapo changamoto hizo chanagamoto zinazowakabili wakazi wa
itenka zinatakiwa kutatuliwa haraka ili kuongeza kasi ya maendeleo ya wananchi.
Katika hali halisi ya kauli mbiyu ya
hapa kazi tu ikisimamiwa ipasavyo na Halmshauri,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkoa
kama serikali ya awamu ya tano inavyoagiza ni wazi kuwa wakazi wa Itenka
wataondokana na matatizo waliyonayo mara kilio cha wananchi kinaposikika.
Comments