Wakazi wa kata ya kazima manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameulalamikia uongozi wa halimashauri hiyo kushindwa kuwapimia viwanja takriban miaka tisa, hali iliyowalazimu baadhi yao kuanza ujenzi wa maeneo hayo bila kupimwa.
MKUU wa mkoa wa Katavi meja generali mstaafu Raphaeli Muhuga amesema chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa tumbaku LATCU kinaweza kupata ufanisi zaidi kama kitaendeleza jitihada zake za kuwekeza katika ujenzi wa majengo kama vitega uchumi.
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini FFDA Kanda ya Magharibi Imeteketeza bidhaa mbalimbali zisizofaa katika matumizi ya binadamu zenye thamani ya shilingi Milioni 6 na laki 5 Ambazo ni sawa na tani 2 zilizoingizwa Kinyemela nchini.
Jumla ya watu watatu kati ya saba waliopatwa na majanga ya moto wamefariki dunia katika matukio sita yaliyotokea yakihusisha majengo na vyombo vya usafiri.