LATCU KATAVI WASHAURIWA KUWEKEZA UJENZI WA MAJENGO KUJIIMARISHA KIUCHUMI
MKUU wa mkoa wa Katavi
meja generali mstaafu Raphaeli Muhuga
amesema chama kikuu cha ushirika cha
wakulima wa tumbaku LATCU kinaweza kupata ufanisi zaidi kama
kitaendeleza jitihada zake za kuwekeza katika ujenzi wa majengo kama vitega
uchumi.
Meja generali mstaafu
Muhuga amezungumza hayo katika kijiji cha Igagala wilaya ya Mpanda mara baada
ya uzinduzi wa soko la Tumbaku uliojumuisha wakulima kutoka vyama mbalimbali
vya ushirika.
Amesema kuwa ubunifu wa
kuwekeza katika majengo ni mfano wakuigwa na mashirika mengine ili kuwaletea tija wakulima.
Aidha kwa upande wake
mwenyekiti wa chama cha ushirika mkoani Katavi Bw Modestus Yamlinga amesema
kuwa jumla ya kilo zaidi ya milioni 9 za Tumbaku zimevunwa katika msimu wa
mwaka 2015/16 kwa mkoa mzima.
Mwandishi: Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments