AHUKUMIWA JERA MIEZI 6 AU FAINI KWA SHAMBULIO LA KUTUMIA MWIKO
MAHAKAMA ya mwanzo mjini Mpanda imemuhukumu mtu mmoja mkazi wa Shanwe kifungo
cha miezi 6 jera au kulipa faini
ya shilingi laki mbili.
Akisoma hukumu hakimu mkazi wa mahakama hiyo mh, sylivesta Makombe amemtaja mshitakiwa kuwa ni Shabani Halfan (28) Mkazi wa shanwe
tarafa ya Misunkumilo ambapo alimshambulia
Cosmas Galimoshi kwa kumpiga na
mwiko sehemu za kichwani na kumsababishia maumivu makali.
Kwa upande wake mshitakiwa
alipopewa nafasi ya kujitetea amekiri kutenda kosa hilo na ameiomba
mahakama impunguzie adhabu kwa kitendo alichokifanya kwani alifanya bila kukusudia na alikuwa ametumia
kilevi.
Mahakama imemhukumu mshitakiwa huyo na kumtaka amlipe bw,Galimoshi fidia za matibabu kiasi cha shilingi elfu hamsini ,na adhabu
hiyo imetolewa ili iwe fundisho kwa
wengine wenye tabia kama hii.
Mwandishi: Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments