WAKAZI KATA YA KAZIMA WALALAMIKIA MANISPAA YA MPANDA KUTOPIMIWA VIWANJA VYAO KWA MIAKA 9 SASA
Wakazi wa kata ya kazima
manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameulalamikia uongozi wa halimashauri hiyo kushindwa kuwapimia viwanja
takriban miaka tisa, hali iliyowalazimu baadhi yao kuanza ujenzi wa maeneo hayo
bila kupimwa.
Wakizungumza katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika makao makuu ya kata hiyo wamedai kuwa
baadhi ya wananchi walijitolea eneo la ekari 63 kwa ajili ya kupimiwa viwanja
ambapo kaya 215 zilichangia kiasi cha shilingi 28,000.
Akijibu malalamiko hayo
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya mpanda Bw. lauter kanoni
amewataka wananchi hao kutoa ushirikiano na kuahidi kushughulikia suala la
upimaji wa eneo hilo lenye mgogoro wa muda mrefu.
Aidha afisa mtendaji wa
Kata ya kazima Bi. Digna Nkana amekiri kuwepo kwa mgogoro huo kwa muda mrefu na
kuongeza kuwa suala hilo limechangia kuzorotesha maendeleo ya kata hiyo.
Mwandishi: Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments