BARABARA YA MPANDA TABORA KUPITIA MTO KOGA YAFUNGULIWA
BARABARA
inayoanzia Mpanda hadi Tabora kupitia daraja la mto Koga imefunguliwa na magari
kuruhusiwa kutumia barabara hiyo kwa safari.
Kufunguliwa
kwa barabara hiyo iliyokuwa imefungwa tangu Januari 28 mwaka huu,kumetangazwa
na Naibu mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia miundombinu nchini Mh:
Suleiman Moshi Kakoso.
Mwenyekiti
huyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini amesema barabara hiyo
imefunguliwa baada ya Kukamilika kwa Ujenzi wa Daraja la Mto Koga lililokuwa
limesombwa na Maji Kufuatia Mvua zilizokuwa zikiendelea Kunyesha na kusababisha
vifo vya watu 10.
Kufunguliwa
kwa barabara hiyo kutaondoa adha kwa wasafiri na wamiliki wa vyombo vya Usafiri
waliokuwa wakilazimika Kupitia Mkoani Kigoma kwenda Mkoani Tabora hali ambayo
imekuwa ikilalamikiwa na Wananchi.
Awali taarifa
za kufunguliwa kwa barabara hiyo zilikuwa zimetolewa Jana na Nasoro
Alfi ambaye ni Kamati ya Usalama
barabarani Mkoani Katavi ambapo alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Meneja wa
Tanroads Mkoa wa Katavi kuwa ujenzi wa daraja la mto Koga umekamilika na magari
yanaruhusiwa.
,Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Nasoro Alfi aliesema barabara hiyo imefunguliwa baada ya
Kukamilika kwa Ujenzi wa Daraja la Mto Koga lililokuwa limesombwa na Maji
Kufuatia Mvua zilizokuwa zikiendelea Kunyesha.
Daraja la
Mto Koga ni Kiunganishi cha Mikoa ya Katavi na Tabora ambapo Kufunguliwa kwake
kutayafanya Mabasi ya abiria kuanza kupitia barabara tofauti na ilivyokuwa
awali ambapo yalilazimika Kupitia Uvinza Mkoani Kigoma.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments