MATUKIO YA MAJANGA YA MOTO YAENDELEA KUTIKISA KATAVI
Jumla ya watu watatu kati ya saba
waliopatwa na majanga ya moto wamefariki dunia katika matukio sita yaliyotokea
yakihusisha majengo na vyombo vya usafiri.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Kaimu
kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani Katavi Inspekta Duma Mohamed
wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake.
Amesema matukio hayo yametokea kwa
kipindi cha mwezi Mei 28 hadi Juni 4 mwaka huu.
Amesema katika matukio hayo,vifo vya
watu wawili na majeruhi watatu vilitokana na gari
walilokuwa wakisafiria kuteketea kwa moto katika mlima Ikondwe.
Aidha Matukio mengine ni mtu mmoja
kufariki dunia baada ya gari kutumbukia mto Kasimba na mwingine kujeruhiwa
baada ya kugongwa na gari huku mtu mwingine akipata hasara ya fedha taslimu
shilingi milioni moja laki moja na elfu hamsini katika soko la samaki
Makanyagio pamoja baada ya chumba na sebule yake na kuunguza karanga gunia moja,kitanda,mchele
debe moja,gunia la mkaa na godoro.
Pamoja na Inspekta Mohamed kuwataka
wakazi Mkoani Katavi kutoa taarifa ya majanga ya moto mapema kwa jeshi la
zimamoto kabla ya athari zaidi kutokea,pia ametoa onyo kali watu kwa wanaotumia
namba 114 maalumu kwa ajili ya kutotoa habari za matukio ya moto kwa kuwatania
jeshi la polisi kinyume na matumizi ya nambahizo huku akisema kuwa watu wawili
mpaka sasa wamefikishwa Polisi kwa
Tuhuma za matumizi mabaya ya namba hizo.
Magari yaliyohusika na ajali ni
pamoja na ajali iliyotokea Juni mosi mwaka huu baada ya kuteketea eneo la mlima Nkondwe na watu
watu 2 kuopteza na majeruhi 3 ambapo
gari halikuokolewa.
Ajali nyingine iliyotokea Mei 28 mwaka huu ilihusisha gari lenye namba za usajili T
725CNZ Toyota Spacila baada ya kutumbukia mtoni na mtu mmoja kufariki dunia.
Aidha Juni Mosi mwaka huu eneo la mpanda hotel mwenesha pikipiki maarufu
Bodaboda aligongwa na gari hali ya majeruhi ambapo mpaka sasa hali yake
inaendelea vizuri katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda.
Mbali na matukio hayo pia matukio ya
ajali ya moto yameripotiwa kutokea kwenye nyumba ya jengo la Tasaff tukio
lililotokea Juni 4 mwaka huu na jengo lingine likiwa ni jengo la Ofsi ya
TANROADS.
Hata hivyo baadhi ya vyanzo vya ajali
hiyo ni wananchi kuchelewa kutoa taarifa mapema katika jeshi la zimamoto.
Hata chanagamoto kwa jeshi la Polisi
wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu duni ya barabara inayowezesha magari ya
zimamoto kupita kufikia eneo la tukio.
Matukio ya majanga ya moto katika
Mkoa wa Katavi yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kusababisha athari kwa
wakazi ikiwemo mali kuungua.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments