WAISLAMU KATAVI WAJIAANDA MFUNGO WA RAMADHANI,WANAKATAVI WAPEWA NENO
Leo ni siku ya mwisho ya siku ya
Shaabani katika dini ya kiislamu ikimaninisha siku ya mwisho kabla ya mfungo wa
siku ya ramadhani kuanza hapo kesho.
Wakati sikukuu hiyo ikitarajia kuanza
kesho,Waislamu Mkoani Katavi wameaswa kutenda yaliyo mema sanjari na kusaidiana
katika shida mbalimbali katika mfungo wa Sikukuu ya ramadhani unaotarajia
kuanza kesho.
Ujumbe huo umetolewa na Shekh wa Mtaa
wa Makanyagio na Imamu wa msikiti Mpanda Hotel ambaye pia ni mjumbe wa kamati
ya Mashehe mkoa wa Katavi Sheikh Said Haruna Omary kwa lengo la kuzungumzia
sikukuu hii ikiwa pia ni kutoa ujumbe kwa waumini wa dini ya kiislamu mkoani
Katavi.
Miongoni mwa mambo ambayo amesisitiza
ni pamoja na kusoma zaidi Quran,kusaidia wenye shida mbalimbali na kutofanya
uharifu.
Halikadhalika baadhi ya waumini wa
dini ya kiislamu wakiwemo Fatma Basesa mkazi wa Mtaa wa Makanyagio na Ramadhani
Shabaani Makame ambao ni miongoni mwa waumini wa dini ya kiislamu pamoja na
mambo mengine wamesema,watanzania wanatakiwa kudumisha amani kipindi cha
ramadhani na kuzingatia mema yaliyofundishwa na mtume mahamad Suraray waray
wasalaam.
Suala la bei za bidhaa nazo
zimezungumza na baadhi ya waislamu huku wakitaka bei kutopandishwa kwani
itakuwa kuwaumiza baadhi ya wasiokuwa na uwezo.
Mfungo wa ramadhani ni miongoni mwa
nguzo kuu tano za dini ya kiislamu.
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments