TFDA KATAVI YATEKETEZA TANI 2 ZA BIDHAA BANDIA ZENYE THAMANI ZAIDI YA SHILINGI MIL.6
Mamlaka ya
Chakula na Dawa nchini FFDA Kanda ya Magharibi Imeteketeza bidhaa
mbalimbali zisizofaa katika matumizi ya
binadamu zenye thamani ya shilingi
Milioni 6 na laki 5 Ambazo ni sawa na tani 2 zilizoingizwa Kinyemela nchini.
Akiongea
wakati wa Uteketezaji wa zoezi hilo
Uliofanyika katika Dampo la kutupia taka la Misunkumilo lililoko Manispaa ya
Mpanda,Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Mahgharibi,Dr.EDdgar Mahundi amesema
bidhaa hizo ziligundulika katika Ukaguzi Uliofanyika Mwezi May mwaka huu Mkoani
katavi.
Amesema kuwa
baadhi ya wlivyoteketezwa ni pamoja na maziwa ya watoto yaliyokuwa
hayajasajiliwa,vyakula vilivyokwisha muda wake,vipodozi na viambata vyake
vilivyokwisha muda wake.
Dr.Mahundi
amesema kuwa bidhaa hizo zina madhara
makubwa kwa mtumiaji pindi anapozitumia kwakuwa hazikuzingatia Ubora Unaotakiwa
ambapo ametoa wito kwa wakazi Mkoani Katavi kuzingatia matumizi ya vitu vyenye
ubora kwa matumizi ya binadamu.
Kwa Upande
wake Mfamasia wa Manispaa ya Mpanda,Victor Kabanga amewataka wananchi kuwa
makini katika kuchunguza tarehe ya kutengenezwa na kuisha kwake kwa
kipindi wanapofanya manunuzi ya bidhaa
yeyote.
Aidha Dr.Herman
Kimwango akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Mpanda,amewataka
wafanya biashara wote kuacha tabia ya kuuza bidhaa ambazo zinahatarisha maisha
kwa watumiaji.
Hata hivyo
amewataka wafanyabiashara kujiandaa kulipia vibali vya biashara zao kuanzia
mwezi Julai kwaka huu kwa wale ambao vibali vyao muda utakuwa umekwisha.
Mwandishi:Vumilia Abel
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments