Posts

DIWANI NA MWENYEKITI WA KIJIJI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO WATAKIWA KUACHA TOFAUTI ZAO ZA KISIASA,WAANDISHI WA HABARI KUFUKUZWA MKUTANO WA HADHARA WANANCHI WANG'AKA

Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imewataka Mwenyekiti wa Kijiji cha Muungano Bw Makalai Njile na Diwani wa Kata ya ibindi Mh, Justin   Shinje Kuachana na Chuki za Kisiasa na badala yake wafanye kazi ya kutatua kero za wananchi wao.

DUKA LATEKETEA KWA MOTO MPANDA,ZIMAMOTO WAENDELEA NA UCHUNGUZI WA CHANZO

DUKA moja limeteketea kwa moto na kuungua baadhi ya bidhaa zilizokuwemo ndani katika maeneo ya soko la Mpanda hoteli mkoani Katavi.

KIKOSI CHA JADI KIJIJI CHA KAWANZIGE MPANDA CHAAPISHWA KUAPMABANA NA UHARIFU

KIKOSI cha ulinzi wa jeshi la jadi maalufu kama sungusungu katika kijiji cha Kawanzige kata ya Kakese manispaa ya Mpanda kimeapa kuendelea na mapambano dhidi ya uhalifu katika eneo hilo.

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA MPANDA USIKU WA KUAMKIA LEO MEI 21,LAPITISHA WATUMISHI 13 KATI YA 16 WALIOKUWA WAMESIMAMISHWA KAZI KUKATWA MISHAHARA KUFIDIA HASARA ILIYOTOKANA NA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA MIRADI ZA MANISPAA,MMOJA AFUKUZWA KAZI,WENGINE WATUPIWA TAMISEMI IWAPANGIE INAKOTAKA MBALI NA MANISPAA

Baraza la madiwani katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ,limepitisha maamuzi   ya kukata mshahara wa watumishi 13 kati ya 16,waliokuwa wamesimamishwa kazi na baraza hiloFebruari 26 mwaka huu,kutokana na tuhuma mbalimbali zikiwemo utumiaji ovyo wa fedha za manunuzi ya gari la kuzoa taka pamoja na ubadhilifu wa fedha ya skimu ya umwagiliaji maji ya kakese ambapo pia watumishi watatu wameshushwa vyeo.

PEMBEJEO ZA RUZUKU MSIMU WA KILIMO 2015/2016 ILIKUWA CHANGAMOTO TUPU KWA WAKULIMA MANISPAA YA MPANDA

WAKATI msimu wa kilimo wa mwaka 2016/2017 ukitarajia kuanza mwezi Septemba mwaka huu,ripoti ya matumizi ya pembejeo Katika msimu uliopita wa 2015/2016 katika Manispaa ya Mpanda imeonesha kuwa ilitumia jumla ya pembejeo 27813 kati ya 32145 zilizoletwa katika Manispaa hiyo zimetumika.

WIZI WA SHUKA,GODORO NA FEDHA VYAMFIKISHA MAHAKAMANI MPANDA

Mtu mmoja mkazi wa kata ya Nsemulwa Wilayani Mpanda amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo Mjini Mpanda kwa kosa la wizi wenye vitu vyenye thamani ya kiasi cha zaidi   ya shilingi laki tatu.

MBUNGE JIMBO LA MPANDA VIJIJINI ALINDIMA BUNGENI DODOMA KUTETEA VITUO VYA AFYA JIMBONI KWAKE

VITUO vya afya vya Mwese,Karema na Mishamo Wilayani Mpanda Vinakabiliwa na ukosefu wa wataalaamu wa afya na gari la wagonjwa-leo Mbunge Jimbo la Mpanda Vijijini Mh.Suleiman Kakoso alindima bungeni kutetea vituo hivyo.