Posts

SERIKALI YAWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI WAKALA WA VIPIMO TANZANIA

Image
Na.Issack Gerald SERIKALI imeamua kuwasimamisha kazi watendaji wawili kutoka Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kuanzia leo ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa mafuta bandarini kutokana na zuio la kufunga kwa mita kwa zaidi ya miaka mitano.                                        Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akipata maelezo bandarini jana Februari 11 kutoka kwa watendaji katika bandari hiyo

MTANDAO WA RADIO ZA JAMII (COMNETA) WAZUNGUMZIA SIKU YA RADIO DUNIANI INAYOFANYIKA FEBRUARI 13,KILA MWAKA.

Image
Na.Issack Gerald-Katavi Mtandao wa Radio za Jamii Tanzania (COMNETA) umetoa rai kwa viongozi wa ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya seriklai za mitaa mpaka ngazi ya taifa,kutumia radio mara kwa mara kwa lengo la kuelimisha na kufikisha ujumbe katika jamii kuliko kiongozi kutumia radio kwa wakati Fulani kwa maslahi binafsi.                                           Mwenyekiti wa Radio za kijamii Bw.Joseph Sekiku hivi karibuni (Aliyesimama) akizungmzia masuala yanayohusu radio za kijamii Jijini Dar es Salaam

HABARI YA ASKARI WA KIKE WA USALAMA BARABARANI KUTEKETEA KWA MOTO NA MPENZI WAKE MKOANI RUKWA HII HAPA,PIA UTAJUA KILICHOTOKEA KWA WATOTO WAWILI WADOGO WALIKUWEMO

Image
Na.Issack Gerald-Rukwa ASKARI wa kike wa Usalama Barabarani, Attuganile Mwakibete (37) na mpenzi wake Sunday Mhagama (36), wameteketea kwa moto baada ya nyumba walimokuwa ndani kuungua.                                                        Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa Jacob Mwaruanda (PICHA NA Issack Gerald)

RIPOTI YA PILI AJALI MTO KOGA : MIILI YA WATU WALIOKUFA MAJI MTO KOGA HADI SASA HAWAJAPATIKANA NA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA.

Image
Na.Issack Gerald-Katavi Miili 5 ya watu waliozama katika mto Koga uliopo mpakani mwa Mkoa wa Tabora na Katavi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji tarehe Januari 26 ,2016 hawajapatikana pamoja na gari walilokuwa wakisafiria.                                             Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk.Ibrahim Hamis Msengi(PICHA NA Issack Gerald)

BWENI SHULE YA SEKONDARI YA KANISA KKKT MPANDA LATEKETEA KWA MOTO,WANAFUNZI 31 WANUSURIKA

Na.Issack Gerald-Mpanda Bweni la wavulana la Shule ya Sekondari ya Sanny inayomilikiwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limeteketekea kwa moto na kuteketeza mali zote za wanafunzi.

OFISA ELIMU AKANUSHA WANAFUNZI 21 KUTIMULIWA WAKITUHUMIWA KUVAA YEBOYEBO AMBAZO PIA ZILICHOMWA MOTO.

Na.Issack Gerald WANAFUNZI wapatao 21 wanaosoma Shule ya Msingi Kilambo cha Mkolechi, Kata ya Kala mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, wamefukuzwa shule kwa muda usiojulikana kwa kuvaa viatu maarufu yeboyebo.

UTAPELI WA FEDHA ZA WALIMU KWA MTANDAO WAENDELEA KULINDIMA KATAVI,C.W.T KATAVI YAWATAHADHARISHA WANACHAMA WAKE

Na.Issack Gerald-Mpanda Chama cha walimu Tanzania (C.W.T) Mkoani Katavi,kimetoa tahadhari kwa wanachama wa chama hicho na watumishi wengine kuwa makini kutokana na utapeli kwa kimtandao ambao umejitokeza ukifanywa na watu wasiofahamika.