BWENI SHULE YA SEKONDARI YA KANISA KKKT MPANDA LATEKETEA KWA MOTO,WANAFUNZI 31 WANUSURIKA
Na.Issack Gerald-Mpanda
Bweni la wavulana la Shule ya
Sekondari ya Sanny inayomilikiwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) limeteketekea kwa moto na kuteketeza mali zote za wanafunzi.
Mkuu wa Shule ya Sanny Sisiter Anna
Usiri amesema kuwa tukio hilo ambalo limetokea leo majira ya saa 12 Alfajiri
hakuna mwanafunzi aliyepatwa madhara kiafya mbali na mali zao zote kuteketea.
Aidha,Mkuu huyo wa shule,ametoa hofu
wazazi wa wanafunzi hao kuwa hawatakosa
mahali pa kulala licha ya bweni lao kuungua ambapo pia wataendelea na
masomo kama kawaida.
Amesema kuwa katika bweni hilo,vitu
ambavyo vimetketea ni magodoro,sare za shule,baadhi ya daftari na vitabu.
Kwa upande wake kiongozi wa bweni
hilo ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule hiyo Bw. Ansel
Felisian amesema kuwa waliamka alfajiri ya saa 12 na kwenda darasani kusoma
ambapo tukio hilo lilijulikana baada ya mwanafunzi wa kidato cha kwanza kutoa
taarifa kwa kiranja huyo baada ya mlinzi wa shule kumwagiza akatoe taarifa juu
ya hali hiyo.
Kwa upande wake Kamanda wa jeshi la
Zimamoto na uokoaji Mkoani Katavi Mrakibu Nestory Kisenya Konongo amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema wamesaidia kuzima moto huo baada ya
kupata taarifa za tukio hilo.
Shule hiyo ina wanafunzi 31 waliokuwa
wakiishi katika bweni hilo huku shule hiyo change yenye kidato cha kwanza hadi
cha tatu ikiwa na jumla ya wanafunzi 66 pekee.
Hata hivyo
chanzo cha ajali hiyo ya moto hakijafahamika na uchunguzi unaendelea kufanyika
Comments