RIPOTI YA PILI AJALI MTO KOGA : MIILI YA WATU WALIOKUFA MAJI MTO KOGA HADI SASA HAWAJAPATIKANA NA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA.
Na.Issack
Gerald-Katavi
Miili 5 ya watu waliozama katika mto
Koga uliopo mpakani mwa Mkoa wa Tabora na Katavi baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kusombwa na maji tarehe Januari 26 ,2016 hawajapatikana pamoja na
gari walilokuwa wakisafiria.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk.Ibrahim Hamis Msengi(PICHA NA Issack Gerald) |
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama Mkoani Katavi ambaye pia ndiye Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Dk.Ibrahim Hamis Msengi wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Ofisini kwake.
Dk Msengi amesema kuwa mpaka sasa
hakuna gari linaloweza kupita kutokana na maji yanayozidi kuongezeka kutokana
na mvua zinazoendelea kunyesha na maji kujaa kwa wingi.
Katika hatua nyingine Dk Msengi
amesema kuwa ukarabati wa barabara ya kutoka Mpanda hadi Tabora unaendelea
kufanyika kwa kiwango cha lami isipokuwa eneo lilipo daraja la mto Koga ndipo
bado kuna utata kutkana na wingi wa maji hayo.
Hata hivyo katika hali ya ukiukwaji
wa onyo linalotolewa na viongozi,kuna watu wanaoendelea kusombwa na maji hayo
kutokana na kudharau katazo hususabi wanaotoka Tabora kuja mpanda.
Comments