UTAPELI WA FEDHA ZA WALIMU KWA MTANDAO WAENDELEA KULINDIMA KATAVI,C.W.T KATAVI YAWATAHADHARISHA WANACHAMA WAKE
Na.Issack Gerald-Mpanda
Chama cha walimu Tanzania (C.W.T)
Mkoani Katavi,kimetoa tahadhari kwa wanachama wa chama hicho na watumishi
wengine kuwa makini kutokana na utapeli kwa kimtandao ambao umejitokeza
ukifanywa na watu wasiofahamika.
Tahadhari hiyo imetolewa na leo na Mwenyekiti
wa C.W.T Mkoani Katavi Mwalimu Gerigori John Mshota wakati akizungumza na
P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda Radio Fm Ofisini kwake.
Amesema kuwa kumezuka makundi ya watu
wanaojitambulisha kuwa ni Viongozi wa C.W.T
kikanda wakiwataka walimu wawape namba za akaunti za benki ili walipwe
mishahara yao.
Aidha amesema kuwa Takribani watu
wanne wakiwemo walimu walitapeliwa
milioni kadhaa na watu wasiowafahamu kwa kutumia mitandao ya
mawasiliano.
Kati ya walimu wawili ambao wamepokea
mawasiliano kutoka kwa matapeli mwezi Februari mwaka huu wakiwa katika harakati
za kutapelewa yumo mmoja wa Shule ya Sekondari Mwangaza iliyopo Manispaa ya
Mpanda.
Amesema kuwa amekuwa akijitambulisha
kuwa yeye ni mlezi wa chama cha Walimu Tanzania C.W.T katika mikoa ya Rukwa,Katavi
na Kigoma.
Kwa upande mwingine chama kimeliomba
jeshi la polisi kusaidia kuwakamata watu wanaojihusisha katika wizi wa kutumia
mitandao.
Mwaka jana mbali na walimu kudai kutapeliwa
wengi wa wananchi walisema kuwa walitapeliwa fedha zao ambapo wimbi hilo
limeendelea kuwakumba waliowengi.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa
C.W.T amewataka walimu waliokuwa wakifanya kazi kwa mkataba kutoka yaliyokuwa
makazi ya wakimbizi na sasa makazi mapya,kuwa wavumilivu wakati madai yao ya
kupatindishwa madaraja na stahiki nyingine zikiendelea kufanyiwa kazi na
mamlaka husika.
Comments