MTANDAO WA RADIO ZA JAMII (COMNETA) WAZUNGUMZIA SIKU YA RADIO DUNIANI INAYOFANYIKA FEBRUARI 13,KILA MWAKA.
Na.Issack Gerald-Katavi
Mtandao wa Radio za Jamii Tanzania
(COMNETA) umetoa rai kwa viongozi wa ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya seriklai
za mitaa mpaka ngazi ya taifa,kutumia radio mara kwa mara kwa lengo la
kuelimisha na kufikisha ujumbe katika jamii kuliko kiongozi kutumia radio kwa
wakati Fulani kwa maslahi binafsi.
Mwenyekiti wa Radio za kijamii Bw.Joseph Sekiku hivi karibuni (Aliyesimama) akizungmzia masuala yanayohusu radio za kijamii Jijini Dar es Salaam |
Rai hiyo imetolewa leo na viongozi wa
mtandao huo Tanzania na umoja wa Mataifa,wakati wa mahojiano na Shirika la
Utangazaji Tanzania TBC kuhusu siku ya radio duniani ambayo inatarajia
kuadhimishwa kesho duniani kote.
Katika mahojiano hayo, Mwenyekiti wa
Mtandao huo Bw.Joseph Sekiku amesema kuwa redio za jamii Tanzania zimesaidia
katika utatuzi wa migogoro baina ya wakulima na wafugaji kwa kuelimisha jamii matumizi bora ya ardhi
pamoja na kuunganisha watawala na watawaliwa kwa lengo la kudumisha amani na
kutatu migogoro hiyo kwa mazungumzo.
Amewaasa viongozi wa umma katumia
vyombo mbalimbali vya habari za kijamii kufikisha ujumbe kwa kuwa radio zipo
kwa ajili kuelimisha,kuburudisha,kuasa na kuhabarisha.
Kwa upande wake Meneja wa Mpanda
Radio Fm ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa
mtandao wa Radio za jamii (COMNETA) Bw.Prosper Laurent Kwigize
amesema kuwa vyuo mbalimbali vinavyoendesha mafunzo ya uandishi,utangazaji na
taaluma yote ya habari kwa ujumla,vinatakiwa kuwa na wakufunzi wenye weledi wa
taaluma ya habari ili kupata watalaamu
wa taaluma hiyo wenye uwezo wa kusaidia jamii na kuepuka kuendelea kuwa
wanafunzi wanapopata kazi katika taasisi.
Aidha Bw.Prosper amesema kuwa
wanasiasa wanatakiwa kutambua umuhimu wa radio hata baada ya kampeni za
uchaguzi kufanyika kuliko kutambua vyombo vya habari wakati wa kampeni za
kusaka kura pekee na baada ya hapo kutorejea kuzungumza na waliompigia kura ili
watambue ni kitu gani kinachoendelea katika kushughulikia ahadi zake.
Meneja wa Mpanda RADIO na makamu mwenyekiti wa Mtandao wa jamii Radio Tanzania Bw.Prosper Laurent Kwigize (Picha na Issack Gerald) |
Katika mahojiano hayo,Bi.Stela Vuzo ambaye
ni Afisa Habari kutoka umoja wa Mataifa aliyeko hapa nchini mbali na kuvitaka
vyombo vya habari kufuata miongozo ya vyomvo vya habari kuepuka uvunjifu wa
amani nchini.
Wakati huo huo,amewataka wanawake na
vijana kutumia vyombo vya habari ikiwemo radio kwa ajili ya kutatua changamoto
zinazowakabili na masuala ya kijasiliamali.
Kwa mjibu wa Shirika la kimataifa la
Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limesema kuwa jumla ya watu milioni 20
duniani Kote wanasikiliza na kutegemea radio katika kuzungumzia masuala mbalimbali
ya kijamii.
Maadhimisho ya siku ya Radio Duniani huadhimishwa
ila mwaka ifikapo Februari 13,ambapo kwa mara ya kwanza maadhimisho haya
yalifanyika mwaka 1946 kote duniani.
Kauli mbiu ya siku ya
Radio Duniani “REDIO KAMA CHOMBO CHA HABARI
WAKATI WA MAJANGA”.
Comments