HABARI YA ASKARI WA KIKE WA USALAMA BARABARANI KUTEKETEA KWA MOTO NA MPENZI WAKE MKOANI RUKWA HII HAPA,PIA UTAJUA KILICHOTOKEA KWA WATOTO WAWILI WADOGO WALIKUWEMO
Na.Issack Gerald-Rukwa
ASKARI wa kike wa Usalama Barabarani, Attuganile Mwakibete
(37) na mpenzi wake Sunday Mhagama (36), wameteketea kwa moto baada ya nyumba
walimokuwa ndani kuungua.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa Jacob Mwaruanda (PICHA NA Issack Gerald) |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda amesema
tukio hilo lilitokea Februari 2, mwaka huu saa 7:15 mchana katika kitongoji cha
Maporomoko, Kata na Tarafa ya Laela Wilaya ya Kipolisi ya Laela.
Inadaiwa kuwa nyumba hiyo iliyoteketea kwa moto ambayo askari
Attuganile alikuwa amepanga vyumba viwili, ni mali Yaiyela Mwamahonje aliyokuwa
akiishi na watoto wake wawili wadogo ambao wamenusurika kufa, licha ya kuwemo
ndani ya nyumba hiyo wakati wa ajali hiyo.
Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Mhagama aliyekuwa rafiki wa
trafiki huyo wa kike, ni mkazi wa Mbeya ambako mkewe anaishi, na alikuwa na
mazoea ya kumtembelea mpenzi wake huyo mara kwa mara.
Inadaiwa askari Attuganile alikuwa ameachana na mumewe wa
ndoa. “Vyumba viwili yaani sebule na chumba walimokuwemo Attuganile na Mhagama
viliwaka moto baada ya jenereta lililokuwa likifanya kazi likiwa sebuleni humo
kulipuka na kuwajeruhi vibaya,” alieleza.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda,Attuganile alifariki dunia
Februari 8, mwaka huu saa 2:30 asubuhi akipatiwa matibabu katika Hospitali ya
Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga.
Mhagama alikimbizwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Mbeya jijini Mbeya ambako alifariki dunia Februari 9, mwaka huu ambapo
hata hivyo kamanda Mwaruanda alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
Chanzo:Jeshi la Polisi Rukwa,endelea
kufuatilia P5
TANZANIA MEDIA
Comments