Posts

MATUKIO YA WIKI MKOANI KATAVI NA TANZANIA KWA UJUMLA KUANZIA JANUARI 18-23,2016.

Tuesday, 19 January 2016 WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI LIKIWEMO SHAMBULIO LA MWILI. Posted By: Issack Gerald | At: Tuesday, January 19, 2016 Na.Issack Gerald-MPANDA VIJANA watatu wakazi wa Mpanda mjini jana wamefikishwa katika mahakama ya Mwanzo mjini Mpanda, wakikabiliwa na shtaka la shambulio la kudhuru mwili.

UDSM YAENDESHA KONGAMANO LA TAFAKURI YA UCHAUZI WA MWAKA 2015,MENGI YAIBULIWA.

Image
Na.Mwandishi wetu-Dar es salaam Watanzania wametakiwa kuacha ushabiki wa vyama vya siasa na badala yake wajikite kutatua matatizo ya kitaifa.                                                       Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Jajji Joseph Sinde Warioba

AFISA MTENDAJI WILAYANI MPANDA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Na.Boniface Mpagape-Mpanda TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Katavi, imemfikisha katika mahakama ya wilaya ya Mpanda   Afisa mtendaji wa mtaa wa Kawajense akikabiliwa na shtaka la kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi elfu thelathini.

WANAFUNZI 1137 WATOKOMEA KUSIKOJULIKANA,AFISA ELIMU KUTANGAZA MSAKO NYUMBA KWA NYUMBA.

Na.Issack Gerald-Nkasi. WANAFUNZI wapatao 1137 kati ya 2257   hawajaripoti shule kuanza kidato cha kwanza mwaka huu katika Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa licha ya serikali kutoa elimu bure.

TAMISEMI YAAGIZWA KUSIMAMIA VIZURI HALMASHAURI

Na.Issack Gerald-Katavi WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ndiyo kitovu cha nchi na kwamba kila Mtanzania ameelekeza jicho lake pale kwa sababu anasubiri kupata huduma ya msingi.

MAAFISA ELIMU NSIMBO WAPEWA SIKU 6 KUHAKIKISHA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUINGIA SEKONDARI WANARIPOTI

Na.Agness Mnubi-Nsimbo. MAAFISA elimu sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo wamepewa siku 6 kuanzia jana, kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza wanaripoti.

JAMII NSIMBO YAOMBWA KUSHIRIKI MATENGENEZO YA MIUNDOMBINU YA BARABARA

Na.Vumilia Abel-Nsimbo JAMII wilayani Nsimbo mkoani katavi imeombwa kushiriki katika matengenezo madogo madogo ya miundombinu ya barabara.