Posts

DAWA ZA MAGONJWA YASIYOKUWA YANAPEWA KIPAUMBELE KUANZA KUGAWIWA KESHO KATAVI

Na.Issack Gerald-MPANDA. JAMII Mkoani Katavi imetakiwa kuzingatia utaratibu wa wataalamu wa afya juu ya matumizi ya dawa za magonjwa yasiyokuwa yanapewa kipaumbele Mkoani   hapa.

WAKAZI MKOANI KATAVI WANAOZUNGUKA HIFADHI WATAKIWA KUTOFANYA SHUGHULI YOYOTE HIFADHINI

Na.Issack Gerald-MPANDA Wananchi wanaoishi karibu na hifadhi mbalimbali Mkoani Katavi wameshauriwa   kutofanya shughuli yoyote ndani ya hifadhi pamoja na   kuzingatia sheria   ya uhifadhi ili kuendelela kuzilinda hifadhi hizo.

WAZAZI,WALEZI KATAVI WAASWA KUWAPELEKA VIJANA WAO KATIKA VYUO KUPATA SOKO LA AJIRA

Na.Issack Gerald-MPANDA WAZAZI na walezi mkoani katavi wameshauriwa kuwapeleka vijana wao katika vyuo mbalimbali vya mafunzo ya ufundi stadi VETA   ili waweze kupata elimu itakayowasaidia kuingia katika soko la ajira ikiwa pamoja na kujiajiri wenyewe pindi wamalizapo masomo yao.

WAKAZI MPANDA WAASWA KUJENGA NYUMBA BORA KUJIKINGA NA MVUA ZA ELNINO

Na.Issack Gerald-MPANDA WAKAZI wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, wameshauriwa kujenga nyumba bora ili kuepukana na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua zinazosadikika kuwa za elnino.

VYAKULA VYA KUTEMBEZA MITAANI VYAPIGWA MARUFUKU MPANDA

Na.Issack Gerald-MPANDA HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda imepiga marufuku   uuzaji wa   vyakula vya kutembeza, kama vile uji, barafu, juice na vyakula vinavyouzwa katika maeneo yasiyo rasmi.

RAIA WAPYA KAMBI YA KATUMBA WAENDELEA KUFURAHIA KUWA WATANZANIA

Na.Issack Gerald-MPANDA MKUU wa makazi ya Katumba yaliyopo wilayani Nsimbo mkoani Katavi   Bw. Athuman Igwe, amesema jumla ya wakimbizi waishio katika wilaya hiyo ni elfu kumi na tisa elfu mia saba sabini na tatu, na waliopata uraia ni sitini na mbili elfu huku walio na vyeti ni hamsini na saba elfu.

WATENDAJI WALIOGOMA KUHUDHURIA KIKAO CHA MKURUGENZI WILAYA YA MPANDA KUKABILIWA NA ADHABU

Na.Issack Gerald-MPANDA HALMASHAURI ya wilaya ya Mpanda imeagiza kuchukuliwa hatua kwa watendaji wa kata na vijiji walioshindwa kuhudhuria kikao cha kazi kilichoitishwa na mkurugenzi bila taarifa.