Posts

MARUFUKU VITUO VYA POLISI KUCHOMWA MOTO

Image
JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limekaririwa likisema linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kuchoma kituo kidogo cha Polisi kilichopo Mofu wilayani Kilombero baada ya kukivamia kwa lengo la kutaka polisi wawape mtuhumiwa wa mauaji ili wamuue. IGP ERNEST MANGU Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alibainisha kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 20, mwaka huu na chanzo ni wanakijiji wapatao 100 kufika katika kituo hicho wakimtaka mtuhumiwa wa mauaji ya mkewe. Tukio la kuchomwa kwa kituo hicho limetokea ikiwa ni siku chache baada ya wananchi wenye hasira kuvamia Kituo cha Polisi Bunju A kilichopo Dar es Salaam na kukichoma moto kwa kile kilichoelezwa ni dereva kumgonga mwanafunzi na kupoteza maisha. Tuseme tu hapa kuwa utamaduni huu wa kuchoma vituo vya Polisi ni lazima ukomeshwe kwa sababu si suluhu la wananchi kupata kile wanachodai zaidi ya kuisababishia Serikali hasara na wakati huo huo kukwamisha huduma nyingine za kijamii. Kama kuna tatizo limetokea ni...

VIJANA WATAKIWA KUTOUZA UTU WAO KATIKA MASUALA YA SIASA

Image
  Vijana katika picha ya pamoja Na.Stanley Msigwa-Mpanda. VIJANA Mkoani Katavi wametakiwa kutouza utu wao kwa kutumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao na badala yake watathmini hatima ya maisha yao.

MATUKIO 6 MAKUU YALIYOTOKEA KATAVI WIKI HILI LA SITA-JAMII YATAKIWA KUWATAMBUA WATOTO WENYE ULEMAVU

Na.Issack Gerald -MPANDA. JAMII Mkoani Katavi imeombwa kutambua uwepo wa watoto wenye ulemavu, ili kuwapatia haki za msingi sawa na  watoto wengine.

MATUKIO 6 MAKUU YALIYOTOKEA KATAVI WIKI HILI LA TANO- 20,162 KATI YA 22,596 WAJIANDIKISHA MAKAZI MAPYA KATUMBA

Image
Wakazi wa makazi mapya ya Katumba wakijandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura Na.Agness Mnubi NSIMBO. WANANCHI 20,162 kati ya 22,596 sawa na asilimia 89 ya wakazi wapya, Wilayani Nsimbo Mkoani Katavi wamejiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.

MATUKIO 6 MAKUU YALIYOTOKEA KATAVI WIKI HILI LA NNE,UBAKAJI WA WANAWAKE,WIZI WAKITHIRI POLISI JAMII WAKACHA ULINZI

NA . Issack Gerald- MPANDA Kukosekana kwa uongozi imara katika sekta ya ulinzi na usalama,kumeababisha vitendo vya wizi na ubakaji kwa wanawake kukithiri katika mtaa wa Msasani Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.

MATUKIO 6 MAKUU YALIYOTOKEA KATAVI WIKI HILI LA TATU KATIKA SISA MGOMBEA UBUNGE CUF MPANDA ASHINDWA KUREJESHA FOMU,AFISA UCHAGUZI ALONGA

NA . Meshack Ngumba- MPANDA Chama cha Wananchi Cuf Kimeshindwa Kurejesha fomu ya Mgombea wa Ubunge Kupitia chama hicho Katika Jimbo la Mpanda Mjini Katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi manispaa ya Mpanda.

MATUKIO 6 MAKUU YALIYOTOKEA KATAVI WIKI HILI LA PILI-WANNE WASHIKILIWA NA POLISI KATAVI KWA KUPORA ZAIDI YA MILIONI 7,SILAHA ZA KIVITA PIA ZAKAMATWA

Na.Issack Gerald - KATAVI Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linawashikilia watu wanne wanaosadikika kuwa majambazi Wilayani Mpanda kwa tuhuma za kujeruhi na kupora kiasi cha shilingi milioni saba.