Posts

UHAKIKI MAJINA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MANISPAA YA MPANDA WAKWAMA,MKURUGENZI KUTOA TAARIFA BAADA YA VIFAA KUAWASILISHWA

NA.Issack Gerald-KATAVI ZOEZI la uhakiki wa taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura limeelezwa kuchelewa kuanza katika Manispaa ya Mpanda kutokana na kucheleweshwa kwa vifaa, zikiwemo mashine za BVR.

WAKAZI NSEMULWA KUWASHTAKI MAAFISA ARDHI MANISPAA YA MPANDA KWA WAZIRI WA ARDHI WAKIPINGA USUMBUFU UPIMAJI WA VIWANJA

NA.Issack Gerald-KATAVI WAKAZI wa mtaa wa Nsemulwa Kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamekusudia kumuita Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kutatua migogoro ya ardhi, wakiwatuhumu maafisa ardhi Wilayani Mpanda kushindwa kutatua migogoro hiyo kwa miaka mitatu sasa.

P5 TANZANIA INAKULETEA WASIFU WA WAGOMBEA KITI CHA URAIS WA TANZANIA,TUNAANZA NDANI YA UKAWA,Mh.Edward Lowassa

Image
  Edward Lowassa aliyeshika maikikrofoni na aliyevaa shati jeupe Edward Ngoyai Lowassa Edward Ngoyai Lowassa Mbunge Bunge la Tanzania Jimbo la uchaguzi Monduli ( Arusha ) Tarehe ya kuzaliwa 26 Agosti 1953 Chama CHADEMA (tangu 28/07/15) Tar. ya kuingia bunge tangu 1990 Alirudishwa mwaka 2005 Waziri Mkuu wa Tanzania Alingia ofisini 2005 Alitanguliwa na Frederick Sumaye Dini Mkristo Elimu yake Chuo Kikuu Digrii anazoshika MA (Development Studies) University of Bath (Uing.) Kazi mwanasiasa Edward Ngoyayi Lowassa (amezaliwa 26 Agosti 1953 ) ni mwanasiasa nchini Tanzania . Alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kumi wa nchi hiyo tarehe 30 Desemba 2005 akajiuzulu tarehe 7 Februari 2008 kwa kutajwa katika kamati ya bunge ya uchunguzi katika utoaji wa tenda kwa kampuni ya ume...

UKAWA WAMPITISHA RASMI LOWASSA KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA

Image
  Edward Lowassa Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa NA MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM Chama cha demokrasia na maendeleo chadema   leo kimemuidhinisha Edward lowasa kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika   mwezi Oktoba mwaka huu.  Wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema uliofanyika   leo Jijini   Dar Es salaam wamepiga kura ya   kuridhia kiongozi huyo aliyejiunga na upinzani akitokea chama tawala CCM kuwa mgombea   Kiti hicho cha   urais   Kupitia chama hicho.  Mwanasiasa huyo Mkongwe hapa Nchini amekuwa   akiyagawa   maoni ya Watanzania tangu akihame chama cha Mapinduzi na Kuhamia chama cha   chadema   tang u vikao vya uteuzi vya ccm   kumpitisha mgombea wa urais kulikata jina lake. Hata hivyo katibu mkuu wa chadema Wilbroad Slaa hakuhudhuria mkutano huo mkuu Kutokana na kuwepo kwa taarifa kuwa hakufurahishwa   na uamuzi wa chadema kumpo...

VIONGOZI WA UMMA TANZANIA WATAKIWA KUWA WAZALENDO KUPITIA WANAOWAONGOZA

  Na.Issack Gerald-KATAVI Viongozi wa umma hapa nchini wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia Uzalendokatika kutekeleza mahitaji ya wanaowaongozana siyo kwa maslahi binafsi.

WENYE SIFA YA KUPIGA KURA KATAVI WATAKIWA KUHAKIKI MAJINA YAO KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA

Image
Nembo ya tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania Na.Tume ya taifa ya Uchaguzi-KATAVI WANANCHI   Mkoani Katavi wametakiwa Kufika katika Vituo vyao walivyojiandikishia   Katika daftari la Mpiga Kura ili kuhakiki taarifa zao   Katika daftari la hilo. Kwa Mjibu wa Tangazo lililotolewa na Tume ya taifa ya Uchaguzi NEC Zoezi hilo limeanza Augost Mosi mwaka huu ili kutoa fursa kwa wananchi waliojiandiksha Kuhakiki taarifa zao zilizokosewa kabla ya Muda wa Kupiga Kura. Jaji mstaafu Damian Lubuva mwenyekiti wa tume ya taifa ya Uchaguzio Tanzania Pamoja na Mkoa wa Katavi Mikoa mingine inayotakiwa kuanza zoezi hilo ni Rukwa,Njombe,Iringa,Mtwara,Lindi,Dodoma,Singida,Tabora na Kigoma.

JAMII KATAVI,KIGOMA YATAKIWA KUWA NA UTAWALA BORA MATUMIZI YA RASILIMALI

Na.Issack Gerald-Katavi Jamii katika mikoa ya Katavi na Kigoma imetakiwa kutumia sera ya utawala bora kutunza vyanzo vya rasilimali katika mazingira yanayoizunguka kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.