JAMII KATAVI,KIGOMA YATAKIWA KUWA NA UTAWALA BORA MATUMIZI YA RASILIMALI
Na.Issack Gerald-Katavi
Jamii
katika mikoa ya Katavi na Kigoma imetakiwa kutumia sera ya utawala bora kutunza
vyanzo vya rasilimali katika mazingira yanayoizunguka kwa manufaa ya vizazi vya
sasa na vijavyo.
Wito
huo umetolewa leo na Kaimu mkurugenzi wa Mpango wa kuhifadhi hifadhi za Gombe,Masilo na Ugala Mary Mavanza katika
kikao cha semina cha utawala bora katika Rasilimali ambacho kimefanyika Mjini
Mpanda kikiratibiwa na taasisi ya Jane Goodal inayojishughulisha na uhifadhi wa
mazingira hapa nchini.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa mradi wa kuhifadhi mazingira wa taasisi ya Jane
Goodal Mkoani Kigoma Emmanuel Mtiti
ameshauri elimu ya utawala bora wa rasilimali na utunzaji wa mazinginra
kutolewa kuanzia ngazi ya mitaa.
Kikao
hicho ambacho kimeanza leo mjini Mpanda kikiwashirikisha wataalamu wa masuala
ya rasilimali na mazingira kutoka Wilayani Mpanda,Nsimbo,Uvinza na Kigoma
kinatarajiwa kufikia tamati Ijumaa ya wiki hii.
Nao
wajumbe walioshiriliki katika semina hiyo wamelisema kuwa viongozi wote wa umma
wakiwemo wakurugenzi,wakuu wa wilaya na viongozi wa dini wanatakiwa
kushirikishwa katika usimamizi wa rasilimali na utuunzaji wa mazingira ili wasaidie
kueneza elimu ya mazingira kwa kiasi kikubwa.
Comments